USHUHUDA: KILICHOMFANYA JOEL LWAGA ATUNGE WIMBO WA SITABAKI NILIVYO


 Bila shaka utakuwa umeshawahi kuusikia au unao kwenye simu au kifaa chako cha kuhifadhia muziki wimbo wa muimbaji wa nyimbo za injili JOEL LWAGA uitwao SITABAKI KAMA NILIVYO. Pamoja na kuwa na melodi nzuri na uimbaji mzuri wa JOEL, wimbo huu una ujumbe wenye nguvu sana na umekuwa faraja kwa watu wengi waliousikia.

Katika ukurasa wake wa instagram, Joel alifunguka kipi kilichosababisha akaandika wimbo huo kama ifuatavyo:
“Ilikuwa ni jioni ya siku ya tarehe 14/2 nikiwa nimekaa ndani mahali nilipokuwa nikiishi (geto) na ni siku ambayo nilijawa na huzuni kupita kiasi, iliyochanganyikana na maswali mengi niliyokuwa nikijiuliza mwenyewe na mengne nikimuuliza Mungu aliyekuwa ķimya kwa kipindi kirefu kwani hyo haikuwa mara ya kwanza kwa mimi kukaa katika hali ya kumuuliza maswali ambayo nitakujuza baadae ni yepi, na yeye(Mungu) kuendelea kuwa kimya tangu mwaka 2010 nilipokuwa form five  aliposema na mimi kwa Mara ya mwisho direct kwa kutumia kinywa changu katika utiisho na ishara za ajabu ambazo sitakuja kuzisahau kamwe.....
Maswali machache kati ya mengi niliyokuwa nikimuuliza ni kama haya
1. kwanini huduma yangu haikui wakati umeshasema na mimi miaka saba sasa imepita na kunipa uhakika kuwa umeniita kukutumikia kwa viwango vikuu vya ajabu, umesema umenipa mataifa kuwa urithi wangu mbona miaka inaenda na sioni kitu?
2. Mbona sioni watu wakiinuka na kunisaidia, mbona wanaishia tu kusema “Joel unaimba vzur sana!” Na wanaishia hapo?
3. Nimekuwa kwny vikundi vingi vya uimbaji, nimekutana na watu wengi na wengi wanasifia nilichonacho lakini mbona yote yanaishia hewani?
4. Mbona wengine wanafanikiwa kirahisi na wengne mbona kiuwezo tu wa kawaida mm nimewazidi lakini mbona wao wanafanikiwa na huduma zao zinakua wanarekodi album na album wanapendwa na watu wengi kila kukicha kwann mimi hayo hayako kwangu?
5. Kwanini maisha yangu yanazidi kuwa duni kila siku pamoja na kwamba umenipa nafasi ya kusoma tena kwa muujiza lakini hali yangu na ya familia yangu (wazazi) ni ngumu kila iitwapo Leo?
6. Kwanini watu ninaojaribu kuwacheki kama vile maprodyuza, wadau mbalimbali wa muziki wanisaidie ili nipige hatua hatua angalau tu nirekodi wote wananitupa kama vle hawaoni nilichonacho?

Nikiwa naendelea kujiuliza na kumuuliza Mungu maswali niliyokuandikia hapo kabla, ghafla siku hyo nilisikia mguso mkubwa na wa tofauti sana ndani yangu kuliko siku nyingnezo na machozi yasiyokoma yakaanza kutiririka usoni kwangu huku sauti haitoki..... Ndipo sauti ikasikika ndani yangu ikisema KUMBUKA WAPI NIMEKUTOA NA KUMBUKA MANGAPI NIMEKUVUSHA, HAYO YATOSHE KWA SASA KWA WEWE KUAMINI KUWA NIMEKUITA NA YA KUWA WEWE NI MWANANGU NA U MTUMISHI WANGU!
Katikati ya hayo machozi na sauti ile iliyokuwa ikisema moyoni mwangu nikarudi nyuma na kukumbuka mengi ambayo Mungu amenivusha LAKINI kubwa kuliko yote ni kuniponya na kaburi wakati nilipoumwa matatizo ya moyo kwa muda wa mwaka mzima nikipoteza fahamu kwa masaa tisa na zaidi kila siku na kusababisha baadhi ya viungo vyangu hasa kutoka kiunoni mpaka miguuni kuanza kupooza (ku-paralyze) hali iliyosababisha kukosa masomo yangu mwaka mzima ya kidato cha sita (kumbuka hii ilitokea muda mfupi tu baada ya Mungu kunipa maono nikiwa form five) nikakumbuka jinsi mama yangu alivyokuwa akipigana kelele za kuomba msaada huku amenibeba mikononi mwake na kukimbia kwa majirani bla viatu ili wamsaidie kuokoa maisha yangu mara nilipokuwa nikipoteza fahamu... hata baada ya jitihada za ufumbuzi za kila namna kushindikana na nikawa mtu wa kubebwa na kutuliwa nisiweze kufanya lolote kwa muda wa Mwaka mzima! Lakini kwa muujiza nisiouelewa mpaka leo, nikainuka kitandani na kwenda shuleni zikiwa zimebaki wiki mbili kufanyika mtihani wa taifa na nikafanya mtihani na kumaliza na nikafaulu vzur na kujiunga na chuo kikuu!
huku machozi yakizidi kunitoka nikakumbuka kuwa(MUNGU) ALIUNUSURU UHAI WANGU LAKINI PIA ALINUSURU ELIMU YANGU! nikalia zaidi....
Katikati ya Nguvu ile Roho wa Bwana akaanza kutoa unabii kupitia kinywa changu ya kuwa sitabaki jinsi nilivyo, mimi ni chombo cha Bwana na Bado mwny chombo anaendelea kukifinyanga ili kifae saana! Hayo niliyokuwa nayapitia na mengine ambayo bado nitaendelea kuyapitia (maana darasa haliishi kila siku tunajifunza) pamoja na kwamba ni magumu kwa hali ya kibinadamu lakini ni ya muda, na Mungu ameyaruhusu ili imani yangu ipimwe, nishinde na kisha niinuliwe.....sina sababu ya kutamani ya wengine wala kujilinganisha kwa sababu wakati wangu upo na ukaribu Nami!
Maneno hayo wakati yakiendelea kutiririka kinywani mwangu na nikiyakiri kwa sauti na kuyaamini moyoni mwangu ndipo Melody nzuri ikaja ikiambatana na hayo maneno na nikaanza kuimba kwa machozi ya furaha na hapo wimbo ukaanza kuzaliwa verse ya kwanza, ya pili, chorus na ghafla nikasimama na kuanza kuzunguka chumba kizima nikiimba 🎶MTETEZI WANGU YU HAI🎶na hapo wimbo ukakamilika (huu ni wimbo ambao sikuwahi kushika Peni na karatasi kuuandika).....

Nikiwa naendelea kuuimba nikaanza kuona na kusikia watu ndani yangu wenye mapito ya kila namna yaliyowachosha mioyo na kuwakatisha tamaa na wamefika mahali hawaamini tena kama kuna mlango wa kutoka hapo walipo Bwana akanena Nami ya kuwa kila atakayesikia maneno ya wimbo huu ukikiri juu ya ushindi wako akayaamini na kuyakiri vivyo hvyo ndivyo uponyaji na ushindi utamjilia juu yake, si kwa sababu ya sauti nzur uliyonayo, si kwa sababu ya mziki mzuri wa vyombo vilivyopigwa vzuri hapana! Ila ni kwa sababu mkono wangu na nguvu yangu vitaenda pamoja na maneno hayo nami nitatenda makuu!.....nilimshukuru Mungu na kuimba wimbo huo mpaka usiku usingizi uliponichukua....”
MWISHO!

2 comments:

  1. Nafarijika sana ninapo sikiliza wimbo huu mungu akubariki sana

    ReplyDelete

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine