SHUHUDA

MICHAEL AELEZA ALIVYOPONYWA UKIMWI:


Mwandishi: Bwana asifiwe!
Michael: Amen!
Mwandishi: Ukiwa mmojawapo wa watu walioponywa UKIMWI, hebu tupatie historia fupi ya maisha yako na jinsi ulivyopokea uponyaji.
Michael: Ahsante sana ndugu mwandishi. Jina langu ni Michael Wanzagi. Nilizaliwa mnamo mwaka 1974 katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. Pia nilipata elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Butiama. Baada ya kumaliza elimu ya msingi nilienda mkoani Mwanza ambako nilikwenda kuishi na dada yangu kwa kusudi la kujiunga na chuo cha ufundi cha VETA. Kama mkristo, nilikuwa nikiabudu katika kanisa la Anglikana.
Mnamo mwaka 1995, nikiwa mkoani Mwanza niliamua kumpokea Yesu Kristo katika maisha yangu ili awe Bwana na Mwokozi wangu. Licha ya kuokoka, sikuwa nimesimama katika wokovu kutokana na aina ya marafiki niliokuwa nao. Ikumbukwe kwamba, “Marafiki wabaya huharibu tabia njema” (1 Wakorintho 15:33 Tafsiri ya King James Version). Kwa kuwa marafiki hawa walikuwa ni watu wenye marafiki wa kike, nilishawishika kuiga mtindo wao wa maisha, yaani, kuwa na marafiki wengi wa kike. Ilikuwa rahisi kwangu kuiga tabia hii kwa kuwa hata kabla ya kuokoka niliwahi kuwa na rafiki wa kike.
Niliambukizwa UKIMWI kutokana na kujihusisha vitendo vya kujamiiana na wasichana. Kweli nilikuwa nimeokoka mwaka 1995 lakini ukweli ni kwamba ni rahisi kuokoka kuliko kutunza wokovu katika utakatifu na haki. Hii ina maana nilikuwa ninachanganya na dhambi ya uasherati. Lakini kuanzia mwezi wa Juni 2006 niliamua kwa dhati kuishinda dhambi iliyokuwa inanizinga upesi katika maisha yangu. Vile vile niliamua kumtafuta Mungu kwa dhati katika maisha yangu katika maombi na kufunga.
Mnamo mwaka 2001, mama yangu mdogo alikuwa anaumwa sana na mimi nikawa miongoni mwa waliotakiwa kumchangia damu. Ilipofika zamu yangu, daktari aliniambia kwamba damu yangu ni nyepesi. Kwa kuwa nilikuwa najihisi kuwa na dalili za UKIMWI, nilimwomba daktari anielezee hali halisi. Daktari hakunificha bali alinieleza hali halisi ya kwamba nilikuwa nimeathirika, yaani, nilikuwa na ugonjwa wa UKIMWI. Sikuweza kuwaambia watu wa familia yangu majibu haya.
Ilikuwa vigumu kwangu kuamini majibu ya daktari kwa kuwa nilijua kwamba UKIMWI hauna dawa na tena huenda huo ungekuwa ndio mwisho wa maisha yangu. Mwaka wa 2001 ulikuwa mgumu sana kwangu kwani baada ya kujua kwamba nina ugonjwa huu, niliamua kununua dawa za usingizi (valium) ili nimeze na kufa bila kupata taabu. Nilinunua vidonge 20 vya valium na nikawa nasubiria dalili za ugonjwa huu wa UKIMWI ziongezeke ili ninywe dawa hizi na kufa.
Nilikuwa na dalili nyingi za magonjwa nyemelezi au magonjwa ya mtegesheo. Hii ni pamoja na majipu kutoka mwili mzima mara kwa mara. Vipele ambavyo vilileta mkanda wa jeshi vilinipata katika mwili wangu.
Vipele hivyo vilinifanya
nijikune sana na kuwa na hali mbaya. Uzito wangu pia ulikuwa unapungua. Homa za mara kwa mara na maleria zilikuwa zinanisumbua mara kwa mara. Wiki mbili kabla ya kupata uponyaji wangu nilipata tena tatizo la mkanda wa jeshi (herpes zosters).
Wakati nasubiri kujiua, nilisikiliza vipindi vya mahubiri ya Mchungaji Zakaria Kakobe katika runinga (TV) ya channel ten. Ni katika kipindi hiki niliwaona watu waliokuwa wakishuhudia kwamba walikuwa wameponywa UKIMWI. Kwa shuhuda za watu hawa, nilivuviwa kuamini kwamba hata nami naweza kuponywa UKIMWI endapo nitamtafuta Mungu kwa bidii.
Tarehe 26 Mei 2006 siku ya Jumatano nilipokuwa nikisikiliza Praise Power Radio, nilipata kumsikia mtumishi wa Mungu, Mtume Prosper Ntepa katika kipindi chake cha saa 2:00 hadi 3:00 usiku. Alipomaliza kipindi chake alisema kwamba kesho yake, yaani, siku ya Alhamisi kutakuwa na ibada ya maombezi kwa watu wenye UKIMWI. Usiku ule wa Jumatano, nilimsikia Roho Mtakatifu akiniasa kuhudhuria ibada hiyo ya maombezi ya watu wenye UKIMWI.
Siku za nyuma nilikuwa nimefuatilia vipindi vyake mara kadha. Wakati Mchungaji Ntepa alipokuwa akifundisha nilidhania ni kijana mdogo sana. Hii ilitokana na namna nilivyoisikia sauti yake. Kipindi hicho Mchungaji Ntepa alikuwa anafundisha somo la funguo saba za kupokea uponyaji pamoja na kutoa shuhuda za watu walioponywa magonjwa wakiwemo watu wenye UKIMWI. Imani yangu ilianza kuimarika mno. Nilianza kuamini kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Shuhuda zile zilinifanya kujua kuwa kwa Mungu yote yanawezekana.
Baada ya kusikia tangazo la semina sikusita tena kuchukua hatua ya kwenda Mhasibu House siku ya tarehe 24 Mei 2006. Niliiona semina ile kuwa ya kipekee sana. Mafundisho yalikuwa na nguvu sana. Kile ambacho Mchungaji Prosper Ntepa alikuwa anafundisha kilikuwa na upako. Ndani ya moyo wangu nilisikia baridi kali. Jambo hili lilinishangaza sana. Pia katika semina hii nilipokea uwezo wa kunena kwa lugha. Huko nyuma nilikuwa sijawahi kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha lakini katika semina hii niliweza kupokea.
Mchungaji Prosper Ntepa alikuwa ametangaza wakati wa semina kwamba siku ya Ijumaa ilikuwa siku maalum ya kuombea waliokuwa wameathirika na virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo nilikwenda bila kukosa katika semina ile. Baadaye Mchungaji Ntepa aliongozwa na Roho Mtakatifu kuwaambia wale wanaohitaji uponyaji wa UKIMWI wabaki baada ya ibada ili aweze kuwaombea maombi maalum. Nilibaki kama watu wengine walivyobaki ili kupata maombezi maalum. Watu zaidi ya 20 walibaki na kuombewa maombi ya uponyaji. Wakati ninaombewa nilisikia nguvu ya Mungu ikipenya katika mwili wangu. Ndani ya moyo wangu nilisikia baridi kali. Jambo hili lilinishangaza sana.
Niliota ndoto siku ya Ijumaa ambayo daktari aliniambia nitoe damu ili kupima maleria. Nilimjibu kuwa sihitaji kupima maleria bali kupima UKIMWI. Ndoto hii ilinionyesha kuwa nilipaswa kwenda kupima UKIMWI.
Kwa hiyo nilijiandaa kwenda kupima siku ya Jumatatu kama Mchungaji alivyotuhimiza kufanya.
Siku ya Ijumaa nilipofika nilienda kwenye ibada hiyo na Mtume Ntepa akaniombea. Kwa kuwa kulikuwa na semina, siku ya Ijumaa mpaka Jumapili nilienda tena kanisani kwa Mtume Prosper Ntepa. Alipotuombea tena siku ya Jumapili, Mtume Prosper alisisitiza kwamba siku iliyofuatia, yaani, Jumatatu twende tukapime ili kuona kama tumeponywa au la. Kabla ya kwenda kupima nilifanya bidii ya kukiri maandiko yaliyomo kwenye karatasi ya Ukiri Maalumu kwa ajili ya uponyaji wa UKIMWI.
Baada ya kupata imani hiyo nilianza kumtafuta Mungu kwa maombi na kufunga mifungo ya kula jioni. Katika maombi yangu ya kufunga nilikuwa nikimwambia Mungu kwamba Zaburi 107:20 inasema, “Hulituma Neno lake, huwaponya, huwatoa katika maangamizo yao.” Nikawa naidai ahadi hii kwa Mungu ili kwamba Mungu alitume Neno lake na kuniponya. Na pia katika Yohana 11:4, Biblia inasema kwamba Yesu alisema kwamba ugonjwa wa Lazaro haukuwa wa mauti bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili Yesu atukuzwe kwa huo. Nilisimamia Neno hili na kusema kwamba UKIMWI si ugonjwa wa mauti bali ni kwa utukufu wa Mungu.
Jumatatu ilipofika, nilikwenda kupima katika hospitali iitwayo Ameni Child Health Care and General Clinic ambayo iko Sinza Palestina - Dar es Salaam. Wakati nakwenda kuchukua majibu ya vipimo vyangu, nilimwambia Bwana kwamba ninaenda kuchukua majibu yanaonesha kwamba sina UKIMWI (HIV Negative) na si vinginevyo.
Nilipoingia kwa daktari, daktari aliniangalia sana na baadaye kunipa hongera kwa kushinda mtihani kwa kuwa majibu yangu yalioonesha kwamba nilikuwa sina tena UKIMWI. Ndipo nilipoinua mikono yangu juu na kumwambia Yesu: “Asante kwa muujiza.” Nilipofika nyumbani nilimpigia simu Mtume Prosper Ntepa na kumwambia kwamba nimepokea uponyaji wa UKIMWI.
Mwandishi: Je unatoa ushauri gani kwa watu wenye UKIMWI?
Kabla ya kutoa ushauri wangu, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mtume Prosper Ntepa na mkewe, Mchungaji Debora Ntepa kwa kunitia moyo wa kusimama katika Neno la Mungu ili niweze kupokea uponyaji wangu. Mungu na azidi kuwabariki na kuwapaka mafuta watumishi hawa.
Aidha, napenda kuwashauri watu wenye UKIMWI kwamba wajitahidi kwenda kwa watumishi wa Mungu wenye huduma sahihi, yaani, watumishi wanaoamini katika nguvu ya Mungu ya uponyaji. Ni vema wafanye hivyo kwani dunia yote inataharuki na kuona kwamba UKIMWI hauna dawa. Lakini yuko Mungu ambaye anaponya magonjwa yote yaliyoshindikana kwa wanadamu ukiwemo UKIMWI.

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine