MFAHAMU PASTOR CHRIS OYAKHILOME PhD (Historia, Ndoa, familia, huduma, nk)


Bila shaka jina Pastor Chris au Christ embassy sio mageni masikioni na kichwani mwako kutokana na umaarufu wa huduma na mchungaji huyo anayesifika kwa kuwa na mafundisho mazuri yenye nguvu na ya kina sana ambayo huleta ufunuo mpya katika neno la Mungu. Wengi tuna vipande vya sauti au video zenye mafundisho yake ambayo yanahamasisha sana na kutupa maarifa ya maisha ya kawaida na ya kikristo.
Leo ni siku ya kumfahamu huyu mtumishi mkubwa wa Mungu pamoja na huduma yake, pia tutaangalia upande wa familia yake na miradi aliyonayo. Upo tayari? Haya twenzetu sasa...
Pastor Chris Oyakhilome (D.Sc., D.D.), ni raisi wa shirika la Believers’ LoveWorld Inc, na huduma ya Christ Embassy yenye makao makuu jijini Lagos, Nigeria. Ni mtumishi wa Mungu aliyejaa roho wa Mungu na mwenye upako wa kiwango cha juu sana pamoja na kipawa cha Uongozi kinachomsaidia sana kuongoza huduma yake iliyosambaa dunia nzima (ya kimataifa). Kama mchungaji, mhudumu wa uponyaji, mfanya-vipindi vya luninga na mwandishi wa vitabu vinavyouzika sana, matamanio ya kila siku ya pastor Chris ni kuwafikia watu wengi zaidi duniani kwa injili na nguvu za Mungu ambayo amekuwa akifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.


KUZALIWA, NDOA, FAMILIA:
Kwa mujibu wa wasifu wake maalum, Pastor Chris Oyakhilome alizaliwa tarehe 7 mwezi Disemba mwaka 1961 na alikuwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya mzee T. Oyakhilome. Alianzisha familia yake kwa kufunga ndoa mwaka 1991 na mchungaji Anita Ebhodaghe na wamebarikiwa kupata watoto wawili wa kike ambao ni Sharon na Charlane.
Baada ya miaka 25 ya ndoa yao, Mke wa pastor Chris Bi Anitha aliamua kutafuta talaka. Hiyo ilikuwa ni tarehe 9 mwezi April 2014 katika mahakama kuu ya familia (Central Famili court) jijini London. Walikuja kuachana/kupeana talaka mwezi Februari mwaka 2016 huku wakiendelea kushirikiana katika kuwalea watoto wao wawili Sharon na Charlane.


MISSION:
Pastor Chris Oyakhilome, anafahamika kwa shughuli zake za kibinadamu na misaada ambazo zinajumuisha kusaidia watu maskini, wagonjwa na wahanga wa majanga mbalimbali kimwili na kiroho. Akiwa na huduma iliyopo kwa zaidi ya miaka 30 sasa, ameweza kuwainua watu wengi kutoka kwenye umaskini, kawaponya magonjwa, na akatoa ujumbe wa tumaini ambao umekuwa ukitangazwa duniani kote kupitia vyombo vya habari vyake. Mradi wake wa Miji ya ndani uliokuwa na kaulimbiu ya “kila mtoto ni wako” imeokoa na kusaidia watoto wengi walio yatima na waliotelekezwa katika miji ya ndani-ndani barani Afrika.


HUDUMA:
Huduma ya Pastor Chris inaongoza project nyingi ikiwemo (Healing school), vijittabu vya kila mwezi vya  Rhapsody of Realities, vitabu vya LoveWorld, na NGO iitwayo Innercity Missions for Children, pia chaneli za televisheni 3 za kikristo ambazo ni: LoveWorld TV, LoveWorld SAT na LoveWorld Plus.
Vipindi vya televisheni za Oyakhilome vimekuwa vikijaa mambo ya uponyaji kwa imani na miujiza inayofanyika katika mikutano mikubwa ambayo inafanywa na hiyo huduma katika nchi mbalimbali, ikiwa na kusanyiko la watu wasiopungua millioni 2.5 katika kila mkusanyiko.

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine