JESHI LA UTURUKI LADAIWA KUSHAMBULIA MAKANISA NCHINI SYRIA


DAMASCUS:
Kanisa nchini Syria limeelezwa kuomba msaada wa kimwili na kiroho baada ya kudaiwa kukithiri kwa mashambulio yanayowalenga kutoka kwa majeshi ya Uturuki. 

Inadaiwa kuwa, majeshi hayo ya Uturuki yamekuwa yakishambulia maeneo ya makanisa katika eneo la Wakurdi nchini Syria ambako kunaelezwa kuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Katika maombi hayo, makanisa yaliitaka jumuiya ya Umoja wa Mataifa kutopuuza mateso wanayopitia kwasababu hali inadaiwa kuelekea kuwa mbaya Zaidi baadaya kundi la wapiganaji wa kiislamu (Jihad) kuungana na Uturuki kuhatarisha usalama wa wakristo kwenye eneo hilo. 

“Sisi viongozi wa makanisa kaskazini mwa Syria katika mji wa Afrin, tunasema kuwa tuko kwenye mashambulio yanayofanywa na Uturuki” ilisomeka moja ya taarifa za makanisa hayo yakiripoti kushambuliwa. 

Iliomgezwa kuwa kwa sasa Maisha ya waumini wakubwa kwa watoto yako hatarini kutokana na mashambulio ya anga yanayoendelea kufanywa na Uturuki, hali iliyosababisha baadhi ya waumini kuanza kukimbia makazi yao. 

“Maisha ya waume, wake na watoto yapo hatarini. Mji wa Afrin sasa uko chini ya Uturuki. Tunaomba kutazamwa na kusaidiwa ulinzi dhidi ya mashambulio haya.” Iliongeza taarifa hiyo.

Mji wa Afrin unadaiwa kuwa na Zaidi ya familia 200 za kikristo na makundi ya kiislamu ndiyo yanaelezwa kuwa na nguvu Zaidi katika mji huo.

SOURCE: UPENDO MEDIA

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine