MAELFU WAPENDEKEZA KUWEPO KWA KUMBUKUMBU YA BILLY GRAHAM MAREKANI


 
Maelfu ya wakristo nchini Marekani wamekusanya sahihi zao kupendekeza kuwepo kwa siku maalum ya kitaifa kila mwaka kwa ajili ya hafla ya kumuenzi mwinjilisti Billy Graham.

Graham, aliyefariki mapema Februari 21, 2018 alikuwa akihubiri katika nchi mbalimbali duniani, na kuwa mwalimu na mhamasishaji wa wanaofanya huduma hiyo katika maeneo mengineyo ikiwemo barani Afrika.

Katika mazishi yake, ilielezwa kuwa watu Zaidi ya 2000 walihudhuria wakiwemo viongozi wakuu wa serikali na familia zao kama Raisi Donald Trump aliyekwenda na mkewe Melania Trump.

Hatua hiyo ya kukusanya sahihi kupendekeza kuwepo kwa kumbukumbu ya Graham ilikuja hivi karibuni ikiongozwa na tovuti ya www.change.org ambapo wakristo Zaidi ya 60,000 tayari wamekwisha saini kuunga mkono pendekezo hilo.

Ilielezwa kuwa baada ya kukusanywa kwa idadi kubwa ya sahihi hizo, zitawasilishwa kwa Raisi Trump ili kusikiliza maamuzi yake juu ya pendekezo hilo. Endapo Trump ataruhusu kumbukumbu ya mwinjilisti huyo, maana yake nchini Marekani kutakuwa na siku maalumu kitaifa kama siku kuu nyingine kwa ajili ya kumuenzi mtumishi huyo wa Mungu.

SOURCE: UPENDO MEDIA

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine