BURUDANI: CECE WINANS, HILLSONG WANG'AA TUZO ZA GRAMMY 2018
cece winans |
Muimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini Marekani mwanamama CECE WINANS pamoja na kundi linalofanya Gospel Rock, na pop la HILLSONG WORSHIP ni moja kati ya wasanii wengi ambao wamefanikiwa kung'aa katika utoaji wa Tuzo kubwa Nchini Marekani zijulikanazo kama GRAMMY AWARDS kwa mwaka huu wa 2018.
Katika Uteuzi wa tuzo hizo, Cece Winans alichaguliwa/alipendekezwa kwenye vipengele viwili ambavyo vyote alishinda. vipengele hivyo ni Wimbo bora wa Gospel ambapo wimbo wake wa "Never have to be alone" ulishinda, Kipengele kingine ni Album bora ya Gospel ambapo Album yake ya "LET THEM FALL IN LOVE" ilishinda na kuwa album bora ya Gospel.
Kundi la Hillsong Worship |
Katika kipengele kingine cha Best contemporary Christian Music Performance/song, kundi la HILLSONG WORSHIP lilishinda kwa wimbo wao wa "what a beautiful name".
Tuzo zingine zinazohusika na muziki wa injili zilikuwa ni Best contemporary Christian Music Album ambayo ilichukuliwa na mtumishi ZACH WILLIAMS na album yake iitwayo "CHAIN BREAKER", na tuzo nyingine ya Best Roots Gospel Album ilienda kwa REBA McEntire na album yake ya "SING IT NOW: SONGS OF FAITH & HOPE"
Muonekano wa tuzo za grammy |
Hongera kwa washindi wote.
Hongera kwa muziki mzuri unaomuinua Mungu wetu.
0 comments: