UONGOZI WA FACEBOOK WAUFUNGA UKURASA WA MASHUJAA WA KRISTO (Warriors for Christ)
NEW YORK:
Uongozi wa mtandao wa kijamii wa FACEBOOK umeamua kuuondoa
ukurasa uliokuwa ukimilikiwa na kikundi cha waumini waliokuwa wakijiita
mashujaa wa kristo (warriors for Christ).
Ukurasa huo uliokuwa na wafuatiliaji
Zaidi ya laki mbili, ukiendeshwa kwa maudhui ya kupinga dhambi ulifungwa hivi
karibuni baada ya kudaiwa kuwa na matumizi ya lugha kali na chuki.
Ilielezwa kuwa asili ya ukurasa huo ilitokana na waumini wa
huduma ya kikristo iliyoko West Virginia nchini Marekani.
Uongozi wa mtandao huo ulieleza kukerwa na tabia ya
wafuatiliaji wa ukurasa huo kutoa lugha za kukejeli na kupinga huduma za utoaji
mimba na vyama vinavyotetea mahusiano ya jinsia moja.
Maneno ya wafuatiliaji hao yaliambatanishwa na ujumbe wa
video wa mchungaji wa huduma yao, Rich Penkoski kuhusu kupinga vitendo hivyo
vilivyotafsiriwa kama uchochezi hivyo Facebook kuufunga ukurasa huo.
Inaelezwa kuwa ukurasa huu uliwahi kufungwa kwa mara ya
kwanza mwezi Disemba 2017 lakini ulifunguliwa muda mchache baada ya watu wengi
kutaka uongozi wa Facebook kutafakari upya maamuzi yao na sasa umefungwa tena.
0 comments: