HUZUNI/PIGO: ASKOFU GWAJIMA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI LEO


Habari za huzuni zilizotufikia hivi karibuni ni kuwa aliyekuwa mama mzazi wa Askofu wa kanisa la Ufufuo Na Uzima, JOSEPHAT GWAJIMA amefariki dunia. Katika post/taarifa aliyoipost katika akaunti yake ya mtandao wa instagram ilieleza kuwa kifo hicho kimetokea mapema leo saa 2 asubuhi na amefariki akiwa na umri wa miaka 84.

Mazishi yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 25/01/2018 katika maeneo ya Salasala, Dar es salaam. 

Pamoja na habari hii kuwa ya huzuni, Askofu Gwajima ameonekana kuwa na tumaini kubwa kuwa mama yake huyo amerudi mbinguni na ni furaha ya ajabu kuwa shujaa yake amerudi mbinguni kwani alikuwa anamtumikia Mungu katika maisha yake. 

Yafuatayo ni maneno aliyoyaandika askofu Gwajima:
"Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam."


Ifuatayo ndio post kamili:


iCHURCH MEDIA tunatanguliza pole zetu kwa familia nzima ya Askofu Gwajima kwa msiba huu. Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. JIna la Bwana lihimidiwe. 

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine