KAA TAYARI KUIPOKEA ALBAMU MPYA YA JENNIFER MGENDI
Muimbaji nguli wa nyimbo za injili Jenipher Mgendi |
Muimbaji mkongwe wa nyimbo za injili Jennifer Mgendi amesema yupo kwenye mchakato wa kuachia albamu yake mpya itakayobebwa na jina “USIPOTEZE LENGO”.
Haya ni maneno aliyaandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook “Kuna watu wanasema heshima pesa, kama kweli heshima ni pesa mbona masumbuko na pesa zake siku moja ali..... nisimalizie uhondo wimbo huu wa Heshima Mungu utapatikana kwenye albamu yangu mpya ya ‘Usipoteze lengo’ nitakujulisha ikikamilika.”
Katika hatua nyingine Jennifer amesema yupo chimbo akiandaa filamu yake mpya itakayoitwa “BABA JACK” ambayo nayo ataiachia hivi karibuni.
0 comments: