HATIMAYE BENKI YA BRITS MONEY YA NABII ANGEL YAPEWA GO AHEAD NCHINI UINGEREZA

Habari zilizotufikia hivi karibuni ni kuwa Benki ya BRITS inayomilikiwa na Nabii Beverly Angel imepata vibali vyote stahiki na kuruhusiwa kuanza kufanya kazi au kutoa huduma za kibenki nchini Uingereza. 

Ikumbukwe kuwa ni zaidi ya mwaka sasa, wamiliki hao wamekuwa wakihangaika kushughulikia vibali hivyo na hapakuwa na urahisi wala mpenyo, jambo ambalo lilifanya mipango yote isimame kwanza. 

Lakini leo katika Ukurasa wake wa mtandao wa instagram, Nabii Uebert Angel alipost picha na maneno yanayoonyesha kufanikiwa kwa jambo hilo. HALELUYA kwa Mungu wetu anayetupigania.

HAYA NI MANENO YA KWENYE HIYO POST (TUMETAFSIRI)

"BREAKING NEWS! Baada ya karibu mwaka wa michakato na vikwazo vya kisheria, TRADEMARK ya Biashara ya #BRITSMONEY imekubaliwa sasa! Kwa hiyo mke wangu @beverlyuangel ambaye ni mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa BRITS MONEY @ britsmoney1 na timu yake ya mabenka wenye ujuzi wa miaka mingi katika benki ni wapo busy kufanya kazi nyuma ya pazia ili kuandaa jukwaa la benki na huduma utakazofurahia. Asante kwa uvumilivu wako. Huu ndiyo wakati hivyo KAA TAYARI!" #britsmoney # launching2018 #unitedkingdom
HII NDIO POST YENYEWE:

Post ya Nabii ya Uebert Angel

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine