MOVIE ILIYOBAMBA: I AM IN LOVE WITH A CHURCH GIRL
Kutana na MILES MONTEGO (JA RULE) kiongozi wa kundi la wauzaji wa madawa ya kulevya mwenye kumiliki kila kitu kama magari, majumba, pesa nyingi mno, wasichana warembo na vingine vyote. MILES ni kama mstaafu ambaye ameamua kutlia na kuanza maisha upya ambapo baada ya muda kidogo anakutana na mdada VANESSA ambaye ni mkristo na jamaa anatokea kumpenda na kutaka kubadilika kabisa ili awe mtu mzuri na kuachana na biashara za magendo. Msichana huyo ambaye alikutana naye katika hafla fupi ya kifamilia ya rafiki yake, MILES anaamua kuanzisha urafiki na kuanza kumfahamu vyema na kugundua kuwa ni mtu wa tofauti ambaye hahitaji aina ya maisha anayoishi yeye (MILES).
VANESSA anacheza nafasi kubwa sana ya kumfundisha MILES na kuhakikisha nkuwa anakuwa na uhusiano mzuri na MUNGU huku akimuonyesha kuwa upendo na rehema za MUNGU zipo kwa ajili yake pia na anaweza kubadilika.
Wakati hayo yakitokea, shirika la uchunguzi la DEA linaanzisha msako na uchunguzi kwa kundi lake MILES kuhusiana na biashara zao za magendo. MILES na wenzanke wakawa wanafuatiliwa mno ingawa majasusi walikuwa wakimshangaa MILES kwani hakuwa akiandamana na wenzake na alibadilika kabisa. Mwisho wa siku wenzake wanakamatwa wakifanya manunuzi na yeye anaponea chupuchupu.
Miles anakutana na mambo magumu yanayomfanya imani yake kwa Mungu ijaribiwe na iimarike pale mama yake anapofariki kwa kansa, lakini pia Vanessa kupata ajali ya gari inayomfanya awe kwenye “COMA” kwa muda mrefu. Alijifunza kuomba.
Filamu inaisha ikimwonesha Vanessa baada ya miaka 3 mbele akiwa kanisani na familia yake, baba yake MILES huku MILES akiwa ni mchungaji na akitoa neno.
Kwa mahitaji ya movie za kikristo wasiliana nasi:
whatsapp 0713861520
text/call 0692408953
0 comments: