MOVIE YA KUANGALIA UNAPOANZA 2018: A WALK IN MY SHOES:
Hii ni movie inayowafanya waangaliaji kutafakari kwamba watajifunza kitu gani iwapo wataingia katika maisha ya mtu mwingine. Mwalimu mwenye msongo wa mawazo katika maisha yake Trish Fahey anashindwa kuelewa upungufu wa juhudi za kusoma na kufaulu za mmoja wa wanafunzi wake na kwanini wazazi wake wanaonekana kutokujali.
Kijana huyo (mwanafunzi) Justine Kremer ambaye ni maarufu shuleni, anayependa kucheza michezo ya skate-board na basketball anapitia mambo mengi yanayosababisha kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake.
Mambo yote yanabadilika baada ya mwalimu TRISH anapokutana na Molly, mtu asiyemjua ambaye anamsaidia kuangalia vitu kwa mtazamo wa tofauti. Baada ya muda kidogo anapata ajali ya gari na anapoamka anajikuta akiwa ndani ya mwili wa mama wa yule mwanafunzi wake ambaye alikuwa akimlaumu na kumhukumu kuwa hamlei vizuri mtoto wake.
Hii hali ya nafsi zao kubadilishana inawafanya wote kujua changamoto alizokuwa nazo kila mmoja wao na kujuta kwanini walikuwa wakihukumiana na kuonana vibaya hapo mwanzo. Pia inamfanya mwalimu TRISH kujua kuwa kuna sababu nyingi mno zinazomfanya mwanafunzi wake awe na hali mbaya darasani na kwanini anashindwa ku-focus pamoja na kumkataza kucheza michezo aipendayo.
Mwisho wa filamu hii kila mmoja nafsi yake inarudi kwenye miili yao ya awali (halisi) na kuwafanya wabadilike na kuanza kuheshimiana, kutokuhukumiana, kupendana, na kusaidiana badala ya kulaumiana.
0 comments: