SERIKALI YAFUNGIA KANISA KWA TUHUMA ZA KUTENGENEZA FEDHA ZA MIUJIZA
Serikali nchini Botswana
imelifungia kanisa la Nabii Shepherd Bushiri kwa kile kinachodaiwa kuwa
anatengeneza “fedha za ajabu”.
Mtumishi huyo alishutumiwa mwaka
uliopita baada ya kubainika kuwa alikuwa akiwatoza kati ya dola 80 hadi 2000
wafuasi wake walikokuwa wakitaka kuhudhuria chakula cha jioni. Nabii Bushiri ni
maarufu kwa mtindo wake wa Maisha ya kifahari huku akiwa na wafuasi wengi
katika kanisa lake.
Bushiri ana wafuasi wengi na
alifanikiwa kujaza watu katika mkesha wa mwaka mpya kwenye uwanja wa mpira wa
FNB ambao ulitumika kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika
ya kusini. Pia mhubiri huyo ana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa chombo cha habari
cha Malawi 24, kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani na limekata rufaa ya
kutaka kuendelea na huduma yake.
Hata hivyo waziri wa mambo ya
ndani wa Botswana, Edwin Batshu alitangaza Aprili mwaka jana kwamba Nabii
Bushiri ambaye sasa anaishi Afrika ya kusini, atahitaji VISA ili kuingia nchini
humo, licha ya raia kutoka Malawi kutohitaji kibali.
Serikali ya nchi hiyo imetangaza
kuwa kanisa hilo litafungwa huku vyombo vya habari vikielekeza kuwa kibali cha
kuendesha kanisa hilo kimefutwa.
0 comments: