TB JOSHUA AZIDI KUFANYA VIZURI MITANDAONI


Mchungaji Mkuu wa kanisa la Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) ambaye pia ni Nabii, T.B Joshua amezidi kufanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufikia idadi kubwa ya watu wanaofuatilia akaunti za huduma yake.
Hayo yamethibitishwa baada ya akaunti ya huduma yao ya instagram kupost taarifa za pongezi na shukrani kwa watu wote duniani wanaowafatilia na wakaweka takwimu zinazoonyesha kufanya vizuri kwa huduma hiyo mitandaoni hasa katika mtandao wa video wa YOUTUBE na wa kijamii wa FACEBOOK.

Katika mtandao wa video wa Youtube, huduma hiyo inayotumia jina la EMMANUELTV, imefuatwa na watu (subscribers) zaidi ya 600,000 huku katika mtandao pendwa wa Facebook ambapo wanatumia jina la TBJMINISTRIES, wamefikisha watu 3,000,000.
Huduma hiyo imekuwa ikijitanua vyema duniani kote na kuifikisha injili ya YESU KRISTO mubashara kupitia chaneli yao ya EMMANUEL TV pamoja na akaunti zao za mitandao ya kijamii na kuleta mguso na shuhuda nyingi kutoka duniani kote namna wanavyobarikiwa, wanavyoponywa na kuwekwa huru kwa jina la YESU.

Makanisa mengi na huduma za Afrika na Tanzania haziamini matumizi ya mitandao ya kijamii na imepiga marufuku waumini wao kutumia mitandao hii. Unadhani ni sahihi? Vipi kanisani kwenu, wanaichukuliaje mitandao ya kijamii? Dhambi/ushetani au FURSA ya kusambaza neno la MUNGU? Na wewe unaichukuliaje pia?
Tuambie au tujibu kwa kuandika ujumbe mfupi kwenda namba 0692408953.

1 comment:

  1. Kwakweli wimbo huu unanibariki sana ,MUNGU aendelee kuwapamoja nawe

    ReplyDelete

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine