MAJOR 1: “HAKUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA UKRISTO NA UMASKINI”

Nabii Shepherd Bushiri
Mnamo 23/12/2017Katika ukurasa wake wa Instagram, nabii Shepherd Bushiri aliandika:

Leo nimechukua muda kuangalia swala la Ukristo na Mafanikio. Nimegundua kuwa mtu asiye mkristo anapofanikiwa ni mara chache sana anakutana na UKOSOAJI wenye uharibifu ndani yake. Lakini anapofanikiwa Mkristo, wakristo wenzake ndio wanakuwa wa kwanza kuruka juu na majungu na ukosoaji mwingi mno. Hii haipo hivi kwa dini zingine kama waislamu na wahindu ambapo mafaniko ya mmoja ni mafanikio ya kila mmoja.

Tuna tatizo gani Wakristo?

Biblia inatuambia kuwa Mungu ana mpango wa kutufanikisha. Na biblia ina maandiko kedekede kuhusu ongezeko la fedha, utajiri na mafanikio. Hii ikimaanisha kuwa katika hali ya kwaida, Mafanikio yanatoka kwa Mungu na kwamba hakuna kitu kibaya wala dhambi kuhusu hilo. Itakuwa dhambi pale tu ambapo mkristo anapokuwa mtumwa wa fedha au anapofanya pesa kuwa mungu kwake. Hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Ni lazima tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake hapo ndipo tutapewa kila tunachohitaji.

Lakini sisi wakristo tumekuja na mtazamo kuwa utajiri unatoka kwa shetani. Tumeamua kuhusianisha utajiri na mambo/vitu vya kiovu/kishetani.

Nasimama kinyume na hiyo mitazamo mibaya kuhusu mafanikio na huduma yangu itaendelea kuwafundisha watu ni namna gani wanaweza kutumia hekima ya kibiblia kufanikiwa na kuutumikia ufalme wa Mungu vyema Zaidi.

Nawatia moyo waumini wangu kufanya kazi kwa bidi katika biashara zao mbalimbali na kufanikiwa ili kutimiza kusudi la Mungu la kutufanikisha. Ni lazima tuushikilie ukweli huo ili tuwe mashahidi wa mipango ya Mungu kwetu.

Na pia ninawashauri watumishi wa Mungu wa kila mahali wasitegemee tu pesa za kanisa na sadaka. Ninawapa changamoto waangalie Zaidi ya madhabahu, wafanye uwekezaji, wafanye biashara na wafanikiwe ili wamtumikie Mungu vyema Zaidi.

Mimi ni ushuhuda uishio juu ya hilo. Biashara zangu zinaendelea vyema kabisa na ninaweza kujilisha, kulisha familia yangu na mamilioni wengine nje huko wenye shida.
Nimetoka kumalizia makubaliano ya dola milioni 10 yanayohusu kinywaji change cha kuongeza nguvu cha Favor na muda si mrefu kinapatikana duniani kote.

Nayasema haya kuwahamasisha  nyinyi waumini wangu kwamba MAFANIKIO NI MPANGO WA MUNGU KWETU na tukifuata anachosema, tutafanikiwa na kudhihirisha kuwa shetani hayupo sahihi."


Source: Instagram account ya Prophet Shepherd Bushiri. 

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine