12 WAFARIKI KATIKA MAANDAMANO YA KANISA KATOLIKI KONGO KUPINGA SERIKALI

 Katika kile kilichoonekana kama kutaka kuitikisa na kuifanya serikali ya nchi ya Kongo inayoongozwa na Raisi Joseph Kabila kutoka madarakani, kanisa katoliki la nchini humo liliitisha maandamano ya kumtaka raisi huyo aachie ngazi. Maandamano hayo yaliyoanza tarehe 31/12/2017 yaligharimu vifo vya watu 12 ambao waliuawa katika maandamano hayo huku 11 wakifa katika mji mkuu wan chi hiyo KINSHASA na mwingine akifa katika mji wa KANANGA.

Kanisa hilo lenye waumini wengi Zaidi katika nchi hiyo Tajiri Zaidi kwa madini lilitoa tamko kwa waumini wake katika parokia 150 kufanya maandamano ya Amani wakiwa na biblia mkononi na misalaba kumtaka Raisi Kabila aachie madaraka kwa kuheshimu mkataba uliosainiwa mwaka mmoja uliopita.
Kabila alitakiwa kuondoka madarakani mwaka 2016 lakini alisogeza muda huo na kusababisha machafuko na ilikubaliwa kuwa uchaguzi ufanyike mwishoni mwa mwaka 2017, hata hivyo uchaguzi huo umeahirishwa hadi Desemba 2018. 



Ikumbukwe kuwa Raisi Kabila alikalia kiti hicho mnamo mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila ambaye aliingia madarakani baada ya kumuondoa Mobutu Sese Seko mwaka 1997.


Source: UPENDO

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine