NEEMA NG’ASHA AACHIA ALBAMU 2 KWA MPIGO:



Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jiji la Mwanza, Neema Ng’asha ameamua kuja kitofauti sana mwaka huu wa 2018 baada ya kuuanza kwa kuachia albamu 2 kwa mpigo ambapo amesema kuwa kufanya hivyo kwake ni baraka.


Katika albamu yake ya kwanza iitwayo TUNAYE BWANA ina jumla ya nyimbo sita ikijumuisha nyimbo kama “mbele ninaendelea”, “tunaye Bwana”, na “wewe ni Bwana”.

Albamu ya pili inajumuisha nyimbo kama “Ebeneza”, “usilie tena”, “nakupenda Yesu wangu”, na “usinipite mwokozi” na ina nyimbo saba.
Pamoja na hayo alisema kuwa kila siku atahakikisha anawapa burudani ya kiroho wapenzi wote wa muziki wake na kuwaomba pamoja waungane naye katika kumsifu Mungu kwa makuu anayotutendea. 


Source: MWANANCHI

Neema Ng'asha akihudumu

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine