WATIMULIWA KANISANI KWA TUHUMA ZA KUWA NA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA


WASHINGTON DC:

Padri wa kanisa katoliki nchini Marekani, amewafukuza kanisani waimbaji wawili wa injili baada ya kupata taarifa kuwa wanajihusisha na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja. 

Akinukuliwa na tovuti ya Christian Today, padre huyo aliyetambulika kwa jina la John Drees, alisema hakukuwa na maamuzi mengine Zaidi ya kuwatimua waimbaji hao.

Alieleza kuwa, vitendo hivyo ni kinyume na mpango wa Mungu na mafundisho ya kanisa hivyo havivumiliki na maamuzi sahihi ilikuwa ni kuwaondoa katika ushirika huo. Uongozi wa juu wa kanisa hilo ulisema kuwa unaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi ya waimbaji hao na maamuzi yaliyofanywa na padre huyo.

Wakati padre Drees akisimamia maamuzi yake kuwa wapenzi wa jinsia moja si halali kuwepo kanisani, kundi la waumini wasiopungua 400 walionekana kupinga msimamo huo.

Inaelezwa kuwa waumini hao wanadai kuwa kitendo kilichofanywa na padri Drees kuwafukuza waimbaji hao kanisani ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kuabudu.

Hayo yanajiri wakati kukiwa na ukinzani kwa serikali za nchi zilizohalalisha mahusiano ya jinsia moja, ambazo hujaribu kusukuma/kulazimisha makanisa kuruhusu ndoa za namna hiyo. 

______________________________________________________________________________

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine