MWANAFUNZI ASHAMBULIWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUKATAA KUBADILI DINI


NAIROBI

Shule ya sekondari ya JAMUHURI nchini Kenya imetajwa kuwa na sintofahamu kwa wakristo baada ya mwanafunzi mmoja kushambuliwa kwa kisu baada ya kukataa kubadili dini kuwa Muislamu.

Ilielezwa kuwa wakati wa usiku, mwanafunzi huyo wa kiislamu alikuwa akiuchambua uislamu na baadaye kuanza kumshawishi aliye jirani naye akane ukristo awe Muislamu na alipokataa ndipo alipomshambulia kwa kisu.

“Kuna mwenzetu yeye ni muislamu alikuwa analazimisha na sisi tulio wakristo tukiri Imani yake, na aliyekataa ndio humchoma kisu na wengine kuwapiga” mmoja wa mashahidi wa tukio hilo alisema.

Taarifa iliyotolewa na tovuti ya christianheadline, ilieleza kuwa shule hiyo iliyoko kaskazini mwa mji wa Nairobi ina ushawishi mkubwa wa makundi ya Kiislamu kutoka nchini Somalia hali inayotishia usalama wa wanafunzi walio waumini wa Kikristo.

Ilielezwa kuwa miezi kadhaa iliyopita, kutokana na ubaguzi uliopitiliza unaofanywa na wanafunzi wa kiislamu dhidi ya wakristo, Uongozi wa shule uliamua kutenga mabafu na vyumba vya maktaba ili kuwaweka katika majengo tofauti kuepuka madhara yanayoweza kuchochewa na ubaguzi huo.

Tovuti ya Morning Star ilieleza kuwa wanafunzi wamekuwa wakinunua visu na mapanga kwa ajili ya kutekeleza uhalifu ndani ya shule hiyo, wakiwalenga waamini wa Kristo.

Katika tukio hilo wanafunzi wengine 15 walijeruhiwa na mamlaka zimeamuru shule hiyo kufungwa wakati polisi wakiendelea na upelelezi kuwabaini wanaochochea vurugu hizo.

SOURCE: UPENDO MEDIA

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine