ASKOFU T.D JAKES AONGOZA WATUMISHI WENGINE DUNIANI KUKEMEA “UTUMWA” NCHINI LIBYA

Bishop TD JAKES
 Askofu na mchungaji mkuu wa kanisa la POTTER’S HOUSE T.D JAKES, ni mmoja kati ya watumishi na wakristo wengi walioguswa na kile kinachoendelea nchini LIBYA kuhusiana na sakata la UTUMWA na BIASHARA YA UTUMWA na kuamua kuliongelea swala hilo kwa masikitiko makubwa sana.
Mkuu huyo wa kanisa hilo lenye makao makuu yake DALAS, TEXAS 28/11/2017 alipost video ya dakika moja kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram ikionyesha alivyoguswa na kuamua kwenda kutembelea baadhi ya maeneo ambayo wakimbizi walikuwa wakiwekwa na kuteswa. 
Video hiyo ilisindikizwa na maneno haya, “Biashara ya utumwa inayoendelea nchini LIBYA na duniani kote ni kitendo cha kikatili kinachotakiwa kusitishwa. Sisi, kama watu inabidi kuungana kusitisha unyama huu kwa maisha ya wanadamu, Haya ni mambo machache unayoweza kufanya:- Tumia sauti yako (Mitandao ya kijamii, jamii yako, nk) kuwafanya watu watambue kinachoendelea. -Unga mkono juhudi za taasisi na mashirika yanayotoa msaada kwa wakimbizi hawa wanaokimbia- Tunatakiwa kusema, HATUTAKIWI KUKAA KIMYA“

Watu mbalimbali mashuhuri na wasio mashuhuri wamekuwa wakipaza sauti kwa vyombo husika ili viingilie kati na visitishe unyama huu unaofanyika ndani ya bara la Afrika huku wengi wakihusianisha na kifo cha aliyekuwa raisi maarufu wa nchi hiyo Muamar Ghadafi kwa kusema kuwa Libya walimgeuka Ghadafi na kuungana na wamarekani kumtoa madarakani na kumuua bila kujua kuwa walikuwa wanampoteza mtetezi wao na shujaa wao. 
Mapema tarehe 30/11/2017 Umoja wa mataifa umetoa tamko la kuagiza mamlaka zote za kulinda haki za binadamu kuchukua hatua mara moja. Haya yamezungumzwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika kikao cha dharura kilichoitishwa kuhusiana na ukatili huu. 
MUNGU AISAIDIE LIBYA,.. 

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine