MAELFU YA WAUMINI WA KKKT waadhimisha miaka 500 ya matengenezo ya kanisa UWANJA WA TAIFA..
Maelfu ya waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani wameshiriki katika ibada maalum ya kuadhimisha miaka 500 ya matengenezo ya kanisa hilo yaliyofanyika huko ujerumani.
Ibada hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jumapili ya tarehe 5 mwezi November iliongozwa na Askofu wa Dayosisi ya mashariki na pwani Dk Alex Malasusa.
Tukio jingine lilioongozana na maadhimisho hayo ilikuwa ni kuwabariki(kipaimara) watoto zaidi ya 4000 kutoka katika sharika mbalimbali za dayosisi hiyo na tukio hili lilifanywa na baba askofu Dk Alex Malasusa.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Profesa Kitila Mkumbo ambaye ni katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji, Fredrick Sumaye (waziri mkuu wa zamani), Detlef Waechter (balozi wa ujerumani nchini) na Isaya Mwita ambaye ni meya wa jiji la Dar es salaam.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa inasema “Wokovu hauuzwi, Uumbaji hauuzwi, Binadamu hauzwi: Tunaokolewa kwa neema ya Mungu.”
Wachungaji mbalimbali wa KKKT dayosisi ya Mashariki na Pwani wakitoa ubarikio (kipaimara) kwa vijana wa kanisa hilo kutoka sharika mbalimbali katika ibada hiyo ya kuadhimisa miaka 500 ya kanisa lao. |
0 comments: