GOSPEL RAPPER LECRAE AFUNGUKA KWANINI KAIITA ALBUM YAKE ALL THINGS WORK TOGETHER



Lecrae Devaughn Moore, anayejulikana kama Lecrae, ni mwanahip hop wa kikristo wa Marekani, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki na muigizaji. Yeye ni rais, mmiliki na mwanzilishi wa studio ya rekodi ya Independent Reach Records, na mwanzilishi mwenza na rais wa shirika lisilo la faida la sasa la ReachLife Ministries. Hadi sasa, ametoa albamu saba na mixtapes tatu kama msanii wa solo, na ametoa albamu za studio tatu, albamu ya remix, na EP moja kama kiongozi wa kundi la hip hop la 116 Clique.

Lecrae ana Album mpya sasa na ameamua kuiita "ALL THINGS WORK TOGETHER" ambayo imepokelewa vyema sana na mashabiki wake ulimwenguni mwote. Lakini juzi kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lecrae aliandika post ndefu kwa mara ya kwanza akielezea hali ngumu ya maisha aliyokuwa akiipitia kuanzia 2015 mpaka 2017 na pia kueleza kwanini album yake ameiita jina hilo.
ALIANDIKA:
"Siandikagi post ndefu ya muda mrefu lakini leo inabidi mkubaliane nami tu. Wakati mwingine unabidi kufunga mdomo na kumsikiliza Mungu. Funga macho yako na uende kwa imani. Kwa mara ya kwanza baada ya muda sasa, nina furaha na nipo huru. Ulichukua muda kufika hapa. Kuanzia 2015-2017 nilikuwa kwenye hali mbaya. Mashaka, hasira, aibu, chuki, kuumia, na kadhalika na kadhalika."

Sijafanya maamuzi ya kuipa albamu yangu jina "ALL THINGS WORK TOGETHER" kwa sababu niliamini ... lakini kwa sababu nilihitaji  kuamini. Mungu ameniruhusu nipate maumivu na kuja upande wa pili bora, na kuwa mwenye hekima, mwenye nguvu, na ujasiri zaidi kama alivyoniumba mimi niwe. Maisha yangu imekuwa safari ya pekee (ningeweza kwenda kutoka Hip Hop Awards hadi Hillsong ndani ya siku) lakini hayo ni maisha yangu lol! Hakuna kujificha au kukimbia kutoka kwao."

"Mimi ninachagua kumfuata Yesu katika kila eneo la maisha yangu. Si rahisi, sio black and white. Kumekuwa na mengi mabaya lakini hata huruma zaidi. Kushindwa kwangu kumesababisha imani kuwa imara. Nina hakika nitaendelea kukua na kubadilisha wengine kama sisi wote tunavyopaswa. Hatimaye ninataka tu kumshukuru kila mmoja wenu ambaye ameniunga mkono kwa yote. Barua zako, ujumbe, sala, na msaada na NEEMA imenipa uzima. Ninakwenda katika sura mpya ya uzima na nina furaha juu ya hilo!" 

Pata muda wa kusikiliza nyimbo za kwenye albamu hii na utupe comment yako juu ya albamu hii pamoja na maisha ya Lecrae kwa ujumla.

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine