MAKAMU WA RAISI WA MAREKANI ATUA ISRAEL KUUNGA MKONO UAMUZI WA TRUMP KUHUSU YERUSALEMU
Siku ya jumapili tarehe 21/01/2018 imekuwa siku ya kihistoria pia baada ya makamu wa raisi wa taifa la Marekani Bwana MIKE PENCE kuwasili nchini ISRAEL kwa ajili ya kuonyesha sapoti ya Marekani katika taifa la Israel.
Mike Pence alipokelewa vyema na waziri mkuu wa Israel Bwana Benjamin Netanyahu.
Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita raisi wa taifa la Marekani Bwana Donald Trump alitoa uamuzi wa kuutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israel na kuahidi kuhamishia ubalozi wake katika mji huo bila kujali mgogoro uliopo juu ya mji huo dhidi ya taifa la Palestina.
Mike Pence alikaririwa akisema "Tunasimama na ISRAEL kwasababu tunaamini katika SAHIHI juu ya VISIVYO SAHIHI, WEMA juu ya UBAYA, UHURU juu ya UDHALIMU"
Makamu huyo bado yupo nchini Israel kwa siku kadhaa. Tutaendelea kukuhabarisha yanayotokea nchini humo.
Usisite kutupa maoni yako juu ya habari hii na ishu nzima ya Mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa taifa la ISRAEL.
0 comments: