Mwaka unapoanza wengi wetu hupanga vitu gani vipya vya kufanya ili kuboresha maisha yetu na kurekebisha makosa ya miaka ya nyuma katika nyanja zote ikiwemo uchumi, mahusiano, masomo, nk. Leo iCHURCH Magazine inakuletea kile ambacho Nabii Shepherd Bushiri maarufu kama "MAJOR 1" ameamua kutuonyesha kuwa ndio mradi ambao anaushughulikia kwa sasa.
Ikumbukwe kuwa Nabii Bushiri amekuwa mmoja wa watumishi wanaopigia kelele swala la watumishi wa Mungu kuishi kwa kutegemea kipato cha madhabahuni tu na kushauri kuwa wanapaswa kujioneza na kuanzisha miradi mingine ili kuhudumia familia zao na kusaidia waumini wao. Na hii ni kwa ajili ya kuwaokoa kutokana na kashfa na majaribu ya kutotumia vyema mapato yatokanayo na sadaka.
Mnamo tarehe 7 mwezi huu wa kwanza Nabii Bushiri kupitia ukurasa wake wa Facebook alipost picha takribani 20 huku akiandika "Part 1 of my personal business, will post part 2 in a few hours time. Don't be intimidated, be inspired. Take notes." akimaanisha kuwa hii ni sehemu ya kwanza ya biashara zanu binafsi, nitapost sehemu ya pili ndani ya masaa machache yajayo. Usitishike, hamasika. Jifunze.
Tumekuwekea baadhi ya picha hizo hapa chini. Enjoy:
|
Nabii Bushiri akiwa na kinywaji chake cha kuongeza nguvu cha FAVOR ambacho
alikizindua mwaka jana. |
|
Nabii Bushiri akiongea jambo na wakandarasi wanaojenga moja ya hoteli zake. |
|
Akifurahia jambo |
|
akiwa na baba yake wa kiroho Nabii Uebert Angel kwenye hiyo miradi |
|
Anamiliki Hoteli za kisasa |
0 comments: