HUZUNI: GOD'S GENERAL C.S UPTHEGROVE AFARIKI DUNIA BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 50 YA HUDUMA

Mtumishi C.S Upthegrove alipomtembelea Nabii T.B Joshua
nchini Nigeria.

Mtumishi wa MUNGU ambaye alipata kuwekwa kwenye list ya watumishi wa Mungu waliotikisa Ulimwengu kwa kuhubiri na kudhihirisha uwepo na nguvu za Mungu, C.S Upthegrove amefariki dunia.

C.S Upthegrove amefariki mnamo jumapili ya tarehe 28 januari 2018 akiwa nyumbani mwake huku akiwa kazungukwa na ndugu, jamaa, na marafiki. 

Mtumishi huyo aliwahi kwenda nchini NIGERIA kumtembelea Nabii TB JOSHUA na kumweleza namna ambavyo amemuona na kuambiwa na Mungu kuja kumkabidhi vitu ambavyo viliachwa na God's General mwingine A.A ALLEN.

C.S Upthegrove amefariki akiwa na miaka 90. Alizaliwa 1928 na amefariki juzi 28/01/2018
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.

Emmanuel TV pamoja na Nabii TB JOSHUA wameandaa video hii fupi:



0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine