MWANAFUNZI ASHAMBULIWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUKATAA KUBADILI DINI
NAIROBI
Shule ya
sekondari ya JAMUHURI nchini Kenya imetajwa kuwa na sintofahamu kwa wakristo
baada ya mwanafunzi mmoja kushambuliwa kwa kisu baada ya kukataa kubadili dini
kuwa Muislamu.
Ilielezwa kuwa
wakati wa usiku, mwanafunzi huyo wa kiislamu alikuwa akiuchambua uislamu na
baadaye kuanza kumshawishi aliye jirani naye akane ukristo awe Muislamu na
alipokataa ndipo alipomshambulia kwa kisu.
“Kuna mwenzetu
yeye ni muislamu alikuwa analazimisha na sisi tulio wakristo tukiri Imani yake,
na aliyekataa ndio humchoma kisu na wengine kuwapiga” mmoja wa mashahidi wa
tukio hilo alisema.
Taarifa
iliyotolewa na tovuti ya christianheadline, ilieleza kuwa shule hiyo iliyoko
kaskazini mwa mji wa Nairobi ina ushawishi mkubwa wa makundi ya Kiislamu kutoka
nchini Somalia hali inayotishia usalama wa wanafunzi walio waumini wa Kikristo.
Ilielezwa kuwa
miezi kadhaa iliyopita, kutokana na ubaguzi uliopitiliza unaofanywa na
wanafunzi wa kiislamu dhidi ya wakristo, Uongozi wa shule uliamua kutenga
mabafu na vyumba vya maktaba ili kuwaweka katika majengo tofauti kuepuka
madhara yanayoweza kuchochewa na ubaguzi huo.
Tovuti ya
Morning Star ilieleza kuwa wanafunzi wamekuwa wakinunua visu na mapanga kwa
ajili ya kutekeleza uhalifu ndani ya shule hiyo, wakiwalenga waamini wa Kristo.
Katika tukio
hilo wanafunzi wengine 15 walijeruhiwa na mamlaka zimeamuru shule hiyo kufungwa
wakati polisi wakiendelea na upelelezi kuwabaini wanaochochea vurugu hizo.
SOURCE: UPENDO MEDIA
0 comments: