MCHUNGAJI ANYONGWA NYUMBANI MWAKE

maelfu ya waandamanaji nchini India wakiandamana kupinga
mauaji ya mchungaji huyu. 

NEW DELHI

Mchungaji wa kanisa moja nchini India amekutwa amekufa baada ya wiki moja kupita akilalamika kuwindwa na wahindi wenye itikadi kali. 

Waumini wa kanisa la MAKNAYEEN alilokuwa akiliongoza mchungaji Gideon Periyaswamy walisema waliukuta mwili wa kiongozi wao ukiwa umening’inizwa na Kamba iliyofungwa kwenye paa la nyumba yake. 

Ingawa taarifa za awali zilieleza kuwa kiongozi huyo alijinyonga, mashuhuda walisema miguu ya mchungaji huyo ilikuwa imepinda, hali inayoonesha alishambuliwa kabla ya kunyongwa. 

Mchungaji huyo alidaiwa kubadili dini kutoka uhindu na kuwa mkristo miaka 25 iliyopita na tangu hapo alikuwa akipata vitisho kutoka dini aliyohama. 
Picha ya Marehemu mch. Periyaswamy akiwa
kama alivyokutwa nyumbani mwake akiwa
amenyongwa.

Inaelezwa kuwa baada ya kubadili dini, miaka 13 baadaye alianza huduma ya uchungaji ambayo aliifanya mpaka umauti ulipomkuta. 

“siku zote wahindu wa hapa hawakupenda maendeleo ya huduma iliyokuwa ikiendeshwa na mch. Periyaswamy, walijaribu kila namna ii kuivuruga.” Alisema Mch. Reuben

Ilidaiwa kuwa, sambamba na kuripoti polisi wiki moja kabla ya kuuawa kwake, Mch. Periyaswamy alishiriki mkutano wa wachungaji ncini humo na kuwaomba wenzake wamuombee kwasababu anakutana na vitisho kutoka kwa wahindu.

“Alituomba tumuombee lakini pia alisema kama Mungu ataruhusu ashambuliwe basi itakuwa ni mapenzi yake kama yalivyotimia kwa Kristo, lakini angependa hata akifa huduma aliyoianzisha iendelee.” Alisema Mch. Reuben 
Marehemu mch. Gideon Periyaswamy enzi
za uhai wake

Polisi walisema wanaendelea na uchunguzi kubaini wahusika wa mauaji hayo na kukiri kuwa ni kweli Mch. Periyaswamy alitoa taarifa ya kuwindwa wiki moja kabla ya kifo chake, hivyo uchunguzi utaanzia hapo. 

Waumini wa kanisa alilokuwa analiongoza Mchungaji huyo walisema kuwa, mara kwa mara wahindi walikuwa wakirusha mawe kanisani hapo na kuvunja vioo vya magari ya wanaokuja kusali na kuonesha kukerwa na huduma hiyo ya kumtukuza Kristo. 

India inashikilia nafasi ya 11 kati ya mataifa 50 yaliyotajwa na taasisi ya World Watch List kuwa hatari kwa Maisha ya wakristo. 




SOURCE: UPENDO MEDIA

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine