NEEMA NG’ASHA AACHIA ALBAMU 2 KWA MPIGO:
Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jiji la Mwanza, Neema
Ng’asha ameamua kuja kitofauti sana mwaka huu wa 2018 baada ya kuuanza kwa
kuachia albamu 2 kwa mpigo ambapo amesema kuwa kufanya hivyo kwake ni baraka.
Katika albamu yake ya kwanza iitwayo TUNAYE BWANA ina jumla
ya nyimbo sita ikijumuisha nyimbo kama “mbele ninaendelea”, “tunaye Bwana”, na
“wewe ni Bwana”.
Albamu ya pili inajumuisha nyimbo kama “Ebeneza”, “usilie
tena”, “nakupenda Yesu wangu”, na “usinipite mwokozi” na ina nyimbo saba.
Pamoja na hayo alisema kuwa kila siku atahakikisha anawapa
burudani ya kiroho wapenzi wote wa muziki wake na kuwaomba pamoja waungane naye
katika kumsifu Mungu kwa makuu anayotutendea.
0 comments: