12 WAFARIKI KATIKA MAANDAMANO YA KANISA KATOLIKI KONGO KUPINGA SERIKALI
Katika kile kilichoonekana kama kutaka kuitikisa na kuifanya
serikali ya nchi ya Kongo inayoongozwa na Raisi Joseph Kabila kutoka
madarakani, kanisa katoliki la nchini humo liliitisha maandamano ya kumtaka
raisi huyo aachie ngazi. Maandamano hayo yaliyoanza tarehe 31/12/2017
yaligharimu vifo vya watu 12 ambao waliuawa katika maandamano hayo huku 11
wakifa katika mji mkuu wan chi hiyo KINSHASA na mwingine akifa katika mji wa
KANANGA.
Kanisa hilo lenye waumini wengi Zaidi katika nchi hiyo
Tajiri Zaidi kwa madini lilitoa tamko kwa waumini wake katika parokia 150
kufanya maandamano ya Amani wakiwa na biblia mkononi na misalaba kumtaka Raisi
Kabila aachie madaraka kwa kuheshimu mkataba uliosainiwa mwaka mmoja uliopita.
Kabila alitakiwa kuondoka madarakani mwaka 2016 lakini
alisogeza muda huo na kusababisha machafuko na ilikubaliwa kuwa uchaguzi
ufanyike mwishoni mwa mwaka 2017, hata hivyo uchaguzi huo umeahirishwa hadi
Desemba 2018.
Ikumbukwe kuwa Raisi Kabila
alikalia kiti hicho mnamo mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent
Kabila ambaye aliingia madarakani baada ya kumuondoa Mobutu Sese Seko mwaka
1997.
Source: UPENDO
0 comments: