WATIMULIWA KANISANI KWA TUHUMA ZA KUWA NA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA
WASHINGTON DC:
Padri wa kanisa katoliki nchini Marekani, amewafukuza
kanisani waimbaji wawili wa injili baada ya kupata taarifa kuwa wanajihusisha
na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.
Akinukuliwa na tovuti ya Christian
Today, padre huyo aliyetambulika kwa jina la John Drees, alisema hakukuwa na
maamuzi mengine Zaidi ya kuwatimua waimbaji hao.
Alieleza kuwa, vitendo hivyo ni kinyume na mpango wa Mungu
na mafundisho ya kanisa hivyo havivumiliki na maamuzi sahihi ilikuwa ni
kuwaondoa katika ushirika huo. Uongozi wa juu wa kanisa hilo ulisema kuwa
unaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi ya waimbaji hao na maamuzi
yaliyofanywa na padre huyo.
Wakati padre Drees akisimamia maamuzi yake kuwa wapenzi wa
jinsia moja si halali kuwepo kanisani, kundi la waumini wasiopungua 400
walionekana kupinga msimamo huo.
Inaelezwa kuwa waumini hao wanadai kuwa kitendo
kilichofanywa na padri Drees kuwafukuza waimbaji hao kanisani ni kuwanyima haki
yao ya msingi ya kuabudu.
Hayo yanajiri wakati kukiwa na ukinzani kwa serikali za nchi
zilizohalalisha mahusiano ya jinsia moja, ambazo hujaribu kusukuma/kulazimisha
makanisa kuruhusu ndoa za namna hiyo.
______________________________________________________________________________
0 comments: