KANISA LA BAPTISTI LACHOMWA MOTO


BISHKEK:

Waumini wa kanisa la Baptisti mashariki mwa Kyrgyzstan wameelezwa kuwa katika hofu baada ya kanisa lao kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

Ilielezwa kuwa redio na televisheni za nchi hiyo ziliripotiwa kutokea kwa tukio hilo ingawa hakuna mtu aliyedhurika na shambulio hilo la moto.

Vyombo vya habari vilisema kuwa kitendo cha kanisa hilo lililopo katika mji wa Kajisay mpakani mwa taifa la China kimesababisha huzuni kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Mamlaka za kulinda usalama zilisema kuwa kulingana na uchunguzi uliofanywa uligundua kuwa wahusika wa tukio hilo ni watu wasiolipenda kanisa hilo na wenye lengo la kutokomeza ukristo katika nchi hiyo ambayo ni ya kiislamu.

Ingawa polisi walitoa matumaini kwa waathirika kuwa watahakikisha wanawatia mbaroni wahusika wa tukio hilo, waumini wa kanisa hilo wameonekana kutilia shaka nguvu ya chombo hicho cha dolakuweza kukamilisha ahadi yake.

“Htuamini kama polisi wataweza kuwatia mbaroni wahusika wa uchomaji moto kanisa letu” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo. 

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine