ASKOFU KKKT KUTEMBEA KWA MIGUU KILOMETA 340
Askofu wa
dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dk.
Emmanuel Makala ataweka rekodi katika utumishi wake kutokana na mpango wake wa
kutembea kilometa 340 kwa lengo la kuujenga Ufalme wa Mungu.
Dk. Makala ataanza
matembezi hayo ya majuma mawili machi 18 katika usharika wa Neema Lamadi na
kumaliza Aprili 1 katika usharika wa Agape uliopo kahama.
Matembezi ya
Askofu huyo yanalenga kukusanya fedha, Zaidi ya shilingi milioni 120 za
maendeleo ya misioni za dayosisi hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali kutokana na kuwa ni eneo ambalo lina mauaji ya albino na vikongwe.
Mojawapo ya
mambo atakayofanya katika matembezi hayo ya miguu ni pamoja na kuendeleza kazi
ya injilli, kukemea mauaji ya albino na kusisitiza watu kufanya kazi kwa bidii.
KILA LA KHERI
ASKOFU.
SOURCE: UPENDO
MEDIA
0 comments: