MAELFU WAPENDEKEZA KUWEPO KWA KUMBUKUMBU YA BILLY GRAHAM MAREKANI
Maelfu ya
wakristo nchini Marekani wamekusanya sahihi zao kupendekeza kuwepo kwa siku
maalum ya kitaifa kila mwaka kwa ajili ya hafla ya kumuenzi mwinjilisti Billy
Graham.
Graham,
aliyefariki mapema Februari 21, 2018 alikuwa akihubiri katika nchi mbalimbali
duniani, na kuwa mwalimu na mhamasishaji wa wanaofanya huduma hiyo katika
maeneo mengineyo ikiwemo barani Afrika.
Katika mazishi
yake, ilielezwa kuwa watu Zaidi ya 2000 walihudhuria wakiwemo viongozi wakuu wa
serikali na familia zao kama Raisi Donald Trump aliyekwenda na mkewe Melania
Trump.
Hatua hiyo ya
kukusanya sahihi kupendekeza kuwepo kwa kumbukumbu ya Graham ilikuja hivi
karibuni ikiongozwa na tovuti ya www.change.org
ambapo wakristo Zaidi ya 60,000 tayari wamekwisha saini kuunga mkono pendekezo
hilo.
Ilielezwa kuwa
baada ya kukusanywa kwa idadi kubwa ya sahihi hizo, zitawasilishwa kwa Raisi
Trump ili kusikiliza maamuzi yake juu ya pendekezo hilo. Endapo Trump ataruhusu
kumbukumbu ya mwinjilisti huyo, maana yake nchini Marekani kutakuwa na siku
maalumu kitaifa kama siku kuu nyingine kwa ajili ya kumuenzi mtumishi huyo wa
Mungu.
SOURCE: UPENDO
MEDIA
0 comments: