FAHAMU DALILI AU VIASHIRIA 10 VYA MWANZO KABLA YA BIASHARA YAKO KUFA

HABARI,
Ni ukweli usiokuwa na nguo kwamba Biashara haiwezi kufa ghafla kama jinsi mtu apatavyo ajali na kufa ilihali ilikuwa katika kiwango cha juu halafu ghala bin vuu inakufa.

Mpaka biashara kufikia kufa ni kwamba kuna muendelezo wa dalili nyingi sana ambazo hupelekea biashara au mfanya biashara kufilisika, ni kama vita kabla ya kuanza huwa kuna viashiria vingi ambavyo huonyesha dalili za vita kuzuka.

1. WAFANYA KAZI WAKO KUKOSA ARI WALA MORALE YA KAZI,

Kitendo cha wafanyakazi kukosa morali/hamasa ya kufanya kazi ni moja kati ya dalili za mwanzo kabisa kabla kampuni yako haijafikia mwisho. Hapa mara nyingi wafanya kazi wanakuwa hawana morale wala ari ya kazi, hawajitumi kufanya kazi kama mwanzo. Hali hii husababishwa namambo mengi sana, na madhara yake huweza kuhamia kwa wateja na hata mali za kampuni.

2. WAFANYAKAZI KUTOTUMIA LUGHA NZURI NA ZA KIBIASHARA KWA WATEJA

Hapa wafanyakazi hufikia hata steji ya kuwagombeza wateja na mara nyingine hata kupiganana wateja.

3. WATEJA KUACHA KUONGELEA MAZURI YA KAMPUNI YAKO/BIASHARA YAKO

Mara nyingi wateja ndio hutumika kutangaza biashara yako kutokana na jinsi wanavyoiona na kuizungumzia kampuni yako kutokana na namna au jinsi wanavyohudumiwa, lakini katika kipindi hiki wateja wanakuwa wanaongelea mabaya ya kampuni yako na si mazuri ya kampuni yako tena. Watakuwa wakilalamika kuhusu huduma zako au bidhaa zako na zaidi kujikita kuongelea mazuri ya mshindani au washindani wako.

4. KASI KUBWA YA KUONDOKA KWA WAFANYAKAZI WAKO MUHIMU,

Ukiona kila kukicha wafanyakazi wako muhimu wanaondoka jua ni moja ya dalili za biashara yako kuelekea kufa. Hapa unakuwa unaondokewa na wafanyakazi ambao ni tegemeo kwa kampuni yako. Katika nyakati kama hizi za ushindani mkubwa wa kibiashara Makampuni mengi huchunguza makampuni yenye changamoto mbalimbali ambazo hupelekea mazingira mabaya ya kazi kwa wafanyakazi mf. wafanyakazi kutolipwa mishahara kwa wakati nk. na kupitia changamoto hizo hutumia sababu hizo kuwayafuta wafanyakazi hao muhimu, kuongea nao na kuwapa ahadi nzuri zenye kuvutia na hatimaye hupelekea wafanyakazi husika kuacha kazi. Mbaya zaidi wafanyakazi hao huweza kutumika kuwachomoa wafanyakazi wengine muhimu kwenye kampuni na kuwaunganisha na mshindani/washindani wako.

5. KUGOMA KWA WASAMBAZAJI WA HUDUMA AU BIDHAA ZAKO

Hawa ni wale waliokuwa wakikusambazia huduma au bidhaa zako na vitu vingine muhimu na kuiwezesha kampuni kufikisha huduma au bidhaabidhaa zaje kwa wateja sasa wanaaza kuacha kutoa huduma kwako au kwa wateja wako. Hii ni moja ya dalili mbaya sana, wasambazaji wako hufikia mahali wakaacha kukusambazia bidhaa/huduma

6. KUPUNGUA KWA FAIDA

Hapa ni biashara kujiendesha kwa faida lakini gharama za uendeshaji kuwa juu kuliko mapato kutokana na MATUMIZI makubwa yanayozidi mapato Mf. Udanganyifu


7. KUSHINDWA KULIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI, KODI NA BILI MBALIMBALI NK.

Hii huwa ni moja ya dalili mbaya kwa biashara yako. Inapofikia ukashindwa kulipa mishahara wafanyakazi kwa wakati, ukashibdwa kulipa Kodi ya ofisi, ukashindwa kulipa bili mbalimbali nk. ni alama kubwa ya kampuni yako kufikia mwisho wake. Madhara au matokeo yake ni kampuni kujikuta ikidaiwa madeni makubwa yasiyoweza kulipika kwa urahisi hali inayoweza kupelekea kufunguliwa kesi mahakamani, kufilisiwa nk.

8. WASHINDANI WAKO KUONGEZEKA

Unapoona washindani wengi sana katika sekta yako au katika kazi ulizokuwa unafanya ni dalili mbaya sana kwa kampuni yako zinazotafsiri kwamba umeshindwa kuitumia vizuri fursa husika na hivyo kutoa mwanya kwa wengine kutumia mapungufu yako, kujiimarisha na kuweza kuchukua sehemu yako. Katika hali hii kama ukishindwa kuchukua hatua za kutosha suluhisho ni kufunga kampuni.

9. SOKO/MASOKO ULIYOKUWA UNAYATEGEMEA KUONDOKA

Kuna kipindi utakuta masoko yako yote tegemezi hayapo tena. Mahali ulipokuwa ukitoa huduma au kuuza bidhaa zako kwa wingi na kupata faida kubwa kwa sasa wahitaji huduma au bidhaa yako tena kwasababu wanahudumiwa na Kampuni nyingine, mshindani wako na mbaya zaidi ikiwa ni kampuni mpya sokoni.

10. WATEJA WAKO MUHIMU WANAHAMIA KWA WASHINDANI WAKO

Wateja uliokuwa ukiwauzia bidhaa au huduma yako kwa sasa hawatumii tena huduma au bidhaa zako na badala yake wanatumia bidhaa au huduma kutoka katika kampuni nyingine ambayo ni mshindani wako mkubwa na wanazifurahia huduma au bidhaa za mshindani wako na kuziponda huduma au bidhaa zako.

HIZI NI BAADHI YA DALILI KUU KABISA ZA BIASHARA YAKO KUFIKIA MWISHO


11. MALALAMIKO JUU YA BIDHAA/HUDUMA ZAKO KUZIDI

Utakuta kila kukicha watu wanaokulalamikia kuhusu bidhaa zako/huduma yako wanazidi,

12. WATEJA WAKO MUHIMU/TEGEMEO KUPUNGUZA KIWANGO CHA MANUNUZI KWAKO

Mfano. Wateja wako muhimu kupunguza ununuzi kwako, walikuwa wananunua kuku 500 sasa wananunua kuku 100 tu, walikuwa wananunua bidhaa za karibia laki moja kwa wiki dukani mwako sasa wananunua za elfu 30,000 tu. Mteja wako muhimu na tegemeo alikuwa ananunua lita30 za maziwa kwa siku kwako sasa ananunua lita5 tu.
Mteja wako muhimu alikuwa akinunua trey100 za mayai kwa mwezi kutoka kwako sasa ananunua trey20 tu.

13. HUWAJALI WATEJA WAKO TENA

Unarudia makosa yaleyale
kila mara na pasipo kuchukua hatua za awali kubadili mfumo na kuyazuia makosa yasiendelee kutumia na badala yake unajikuta unarudia makosa yaleyale kila siku. Hapa ujue ni kwamba hii ni dalili mbaya sana kwa afya ya biashara yako.

14. KUWALIPA WATU/KAMPUNI/TAASISI ZINAZOKUDAI NJE YA MUDA MLIOKUBALIANA.

Ukianza kuwalipa watu wanaokudai nje ya muda wa makubaliona au kuwasumbua malipo yao kutokana na visingizio mbalimbali hiyo nayo ni ishara mbaya sana kwani kitakachofuata ni hao wadeni wako kushindwa kufanya kazi tena na wewe hata pindi utakapokuwa n uhitaji bado watashindwa kukusaidia.

15. KUSHINDWA KULIPA MIKOPO YA BENKI

Kuanza kuuza baadhi ya mali za kampuni yako ili kukidhi mahitaji yako. Ikifikia wakati ukaanza kuuza baadhi mali za kampuni yako ili kuendeshea kampuni yako basi hapo ujue kampuni inakata roho polepole na ujiandae kisaikolojia.

16. KUBADILI JINA LA KAMPUNI GHAFLA

Hii pia ni moja ya dalili mbaya sana kwa kampuni au biashara yako kwani kwa namna moja au nyingine inapelekea wateja ambao kwa sababu zao mbalimbali huamua kuchana na huduma au bidhaa zako kwa kuhisi kwamba si halisia walizozoea kuzitumia kutoka katika kampuni yako.

17. KUENDELEA KUPATA HASARA KWENYE KAMPUNI YAKO

"The aim of any business is for the owner to get/gain profit" Lengo la biashara yoyote ni kwa mmiliki kupata faida. Inapofikia wakati ambapo kampuni inakuwa ikijiendesha kwa hasara basi busara na hekima kubwa inahitaji ka.

Kuna wakati unaweza kukuta solution pekee ya kunusuru kampuni yako ni kuiuza au kuifunga kabisa, na hii ni ili ikunusuru na madeni zaidi, maana yake unaweza kuta the more unavyo operate ndo the more unavyo pata hasara na kutengeneza madeni mengi sana ambayo yatakuja kukuwia vigumu kuyalipa

Washauri wanaweza kukuambia hapa no way out ni kufunga au kuuza kampuni, unaweza kukuta kampuni iko katika hali ambayo haitaweza kukopesheka kamwe, wala kujiendesha tena wewe utafanyaje? competetitor wanakuwa wengi sana, wateja wamekukimbia, wafanyakazi wanakudai mishahara ya miezi kadhaa au wameondoka karibia wote, umeshindwa kurudisha mikopo ya mabenki nk.

Hata makampuni makubwa yanayofilisika si kwamba unakuta hayana kitu kabisa bali hufikia hapo ili kujinusuru na matatizo zaidi. Kufunga biashara si kushindwa, unafunga unakaa unatafakari unakuja na mbinu mpya, na hii huwa ni moja ya sehemu ya kujifunzia ili usije fanya makosa tena.

Lewis Mangula
© 2018

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine