NABII BUSHIRI AELEZA NAMNA ALIVYOKOSWAKOSWA KUOA MKE ASIYE SAHIHI



Siku ya Leo, Nabii Shepherd Bushiri " MAJOR 1" ameamua kutueleza stori yake ya mahusiano kidogo huku akigusia namna ambavyo ilibakia kidogo sana aoe mwanamke ambaye hakuwa chaguo la Mungu kwake.

Haya ameyaandika kupitia ukurasa wake wa instagram wakati akimshukuru Mungu kwa ajili ya mke wake MARRY BUSHIRI ambaye amekuwa mke mwema kwake na mama bora wa watoto wake. Lakini pia alitumia ujumbe huo kuwapa hamasa na kuwafariji watu wanaomfuatilia na wanaomuomba Mungu kila kukicha kuwa na wao Mungu atawapa na wasiwe na papara. Haya ni maneno yake: 

"Nilipoanza huduma yangu, mahali fulani huko mji wa Mzuzu nchini Malawi, kulikuwa na mwanamke ambaye nilifikiri Mungu alitaka nimuoe. Niliomba, kufunga na kuombea kwa siku nyingi, lakini sikupata jibu lolote kutoka kwa Mungu kuhusu kile nilichofikiri kilitoka kwake. 

"Sikuchoka. Niliendelea kuomba bila kujua kwamba mwanamke huyo alikuwa tayari amechumbiwa na mtu fulani kwa miaka mingi na harusi yao ilikuwa ikikaribia. Nilivunjika moyo, nilijiuliza: Je, ile ndiyo sababu Mungu hakuweza kujibu sala zangu? 

"Miezi michache baadaye, Mungu alinionyeshe uzuri, mwanamke mwenye ujasiri ambaye, leo, siwezi kuacha kukubali jinsi alivyo mke mzuri. 

"Ninamshukuru Mungu kwa maombi hayo ambayo hakuyajibu. Maombi ambayo yangeweza kusababisha ukatishaji tamaa mkubwa. Wewe, pia, una maombi mengi ambayo hayajajibiwa. Usitikisike. Kuwa mtulivu, mngojee Mungu, kukataa kwa Mungu ni sababu tu ya kurejea kwa kitu kikubwa na bora zaidi."

Vijana mpo? Mmepata somo hapo?


1 comment:

  1. Hello,writer am much interest with your new but can you alter the coralyou are using to write instead of using red you can use black.Because for those who has a problem of eyes like me i can`t read it.
    That is advising not commanding.

    ReplyDelete

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine