MAJOR 1: “HAKUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA UKRISTO NA UMASKINI”
Nabii Shepherd Bushiri |
Mnamo 23/12/2017Katika ukurasa wake wa Instagram, nabii
Shepherd Bushiri aliandika:
“Leo nimechukua muda kuangalia swala la Ukristo na
Mafanikio. Nimegundua kuwa mtu asiye mkristo anapofanikiwa ni mara chache sana
anakutana na UKOSOAJI wenye uharibifu ndani yake. Lakini anapofanikiwa Mkristo,
wakristo wenzake ndio wanakuwa wa kwanza kuruka juu na majungu na ukosoaji
mwingi mno. Hii haipo hivi kwa dini zingine kama waislamu na wahindu ambapo
mafaniko ya mmoja ni mafanikio ya kila mmoja.
Tuna tatizo gani Wakristo?
Biblia inatuambia kuwa Mungu ana mpango wa kutufanikisha. Na
biblia ina maandiko kedekede kuhusu ongezeko la fedha, utajiri na mafanikio.
Hii ikimaanisha kuwa katika hali ya kwaida, Mafanikio yanatoka kwa Mungu na
kwamba hakuna kitu kibaya wala dhambi kuhusu hilo. Itakuwa dhambi pale tu
ambapo mkristo anapokuwa mtumwa wa fedha au anapofanya pesa kuwa mungu kwake.
Hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Ni lazima tuutafute
kwanza ufalme wake na haki yake hapo ndipo tutapewa kila tunachohitaji.
Lakini sisi wakristo tumekuja na mtazamo kuwa utajiri
unatoka kwa shetani. Tumeamua kuhusianisha utajiri na mambo/vitu vya
kiovu/kishetani.
Nasimama kinyume na hiyo mitazamo mibaya kuhusu mafanikio na
huduma yangu itaendelea kuwafundisha watu ni namna gani wanaweza kutumia hekima
ya kibiblia kufanikiwa na kuutumikia ufalme wa Mungu vyema Zaidi.
Nawatia moyo waumini wangu kufanya kazi kwa bidi katika
biashara zao mbalimbali na kufanikiwa ili kutimiza kusudi la Mungu la
kutufanikisha. Ni lazima tuushikilie ukweli huo ili tuwe mashahidi wa mipango
ya Mungu kwetu.
Na pia ninawashauri watumishi wa Mungu wa kila mahali
wasitegemee tu pesa za kanisa na sadaka. Ninawapa changamoto waangalie Zaidi ya
madhabahu, wafanye uwekezaji, wafanye biashara na wafanikiwe ili wamtumikie
Mungu vyema Zaidi.
Mimi ni ushuhuda uishio juu ya hilo. Biashara zangu
zinaendelea vyema kabisa na ninaweza kujilisha, kulisha familia yangu na
mamilioni wengine nje huko wenye shida.
Nimetoka kumalizia makubaliano ya dola milioni 10 yanayohusu
kinywaji change cha kuongeza nguvu cha Favor na muda si mrefu kinapatikana
duniani kote.
Nayasema haya kuwahamasisha
nyinyi waumini wangu kwamba MAFANIKIO NI MPANGO WA MUNGU KWETU na
tukifuata anachosema, tutafanikiwa na kudhihirisha kuwa shetani hayupo sahihi."
Source: Instagram account ya Prophet Shepherd Bushiri.
0 comments: