BOT YAIFUNGIA BENKI YA EFATHA NA NYINGINE 4
Gavanna Wa benki kuu, prof. Benno Ndullu akiongea na waandishi wa habari hapo |
Benki zingine zilizokutana na adhabu hiyo ni COVENANT BANK FOR WOMEN (TANZANIA) LIMITED, NJOMBE COMMUNITY BANK LIMITED, KAGERA FARMERS COOPERATIVE BANK LIMITED, na MERU COMMUNITY BANK LIMITED.
Taarifa hiyo imetolewa jana kwa vyombo vya habari na benki hizo zilifungwa mara moja ikiwa ni pamoja na tovuti zao pia.
Chanzo cha agizo hilo imeelezwa kuwa ni kushindwa kufikia makubaliano na sheria mpya ambayo iliziagiza benki zote Tanzania kuongeza mitaji yao kufikia BILLIONI 2 kutoka MILLIONI 200 kama ilivyokuwa awali.
Akizungumza Leo jijini dar es salaam Gavanna Wa benki kuu, prof. Benno Ndullu ametoa taarifa hiyo wakati akianga na kumkabidhi nafasi yake alio nayo gavanna mpya Prof. Florence luoga, amesema benki hizo zilipewa muda Wa miaka 5 ili kuongeza mtaji kufikia kiwango kipya ambapo muda Huo uliisha juni 2017 na muda huo kuongezwa hadi kufikia disemba 31, 2017.
Prof. Ndullu amesema benki tano kati ya nane zilishindwa kuandaa na kuwasilisha benki kuu mpango mkakati unaokubalika Wa kuongeza mtaji na pia kuzifanya benki hizo kuwa endelevu kutokakana na kutotimiza matakwa ya kisheriaya kuwa na mtaji kamili na Wa kutosha hivyo imeamua kuzifunga na kusitisha shughuli za kibenki benki hizo.
Mtume na Nabii Josephat Mwingira akiwa na mke wake katika ibada zao |
Muonekano wa Benki ya EFATHA ndani kabla haijafungiwa |
0 comments: