PAUL CLEMENT : MSINIITE SUPERSTAR

Moja kati ya mambo ambayo yametrend leo ni pamoja na kile alichoamua kuandika muimbaji maarufu wa nyimbo za injili PAUL CLEMENT katika ukurasa wake wa mtandao wa instagram. Paul ameamua kufunguka na kuwaambia wadau wake kuwa hataki wamuite "superstar" na ni bora wakikutana naye wamuite tu jina lake.


Haya ni maneno yake:


"Ni nani aliyekuambia kuwa mimi ni super star?......mbona unaniita super star,mtu mkubwa na majina mengi yenye utukufu mwingi..Ni bora uniite jina langu kuliko kuniita super star...sikuzaliwa ili nije kustarehe,sikuzaliwa ili nije kuabudiwa,sikuzaliwa ili Watu wanitetemekee,Sikuzaliwa ili Watu wanitumikie ila mimi niwatumikie wao kwa kile ambacho(MUNGU AMENIPA) ninacho.kwa kusema hivi sio kwamba najishusha ili nionekane mnyenyekevu hapana ila nakumbuka niliambiwa niende ulimwenguni kwote nikaihubiri injili kwa kila kiumbe. .sidhani kama nina muda wa kupoteza wa kukaa kustarehe sababu tu umeniambia mimi ni super star.Rafiki yangu wa zamani alipotea njia kwa sababu neno super star lilimpendeza.Dunia itanitambua tu wala sihitaji kupambana ila itanitambua kwa injili ambayo nimechagua,pia nimekubali kuipeleka .inanitosha kujua kuwa mimi ni NURU ya ulimwengu na kuwa mimi ni mji uliojengwa juu ya mlima kamwe hauwezi kusitirika.
Jina langu sio super star........jina langu ni zaidi super star.....kwa sababu super star ana mwisho."


post ya paul Clement 
Unaona yupo sahihi?
Unalichukuliaje swala hili?
Tupe maoni yako.
Comment.................

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine