BREAKING NEWS: MTUMISHI WA MUNGU NA MWINJILISTI WA KIMATAIFA BILLY GRAHAM AFARIKI DUNIA
NORTH CAROLINA, MAREKANI:
Mhubiri wa Kimataifa, Mchungaji Billy Graham(99) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake
Mchungaji huyo amefikwa na mauti baada ya kuugua magonjwa kadhaa ikiwemo Saratani ya tezi dume na Kiharusi
Graham amewafikia watu wengi na injili kupitia Tv na alikuwa mtumishi wa kwanza kutumia njia hiyo. ..
Alizaliwa 1918 na kukulia kitongoji cha Charlote, North Carolina na aliamua kuwa mkristo anayemaanisha akiwa na miaka 16 baada ya kusikia injili kutoka kwa mwinjilisti aliyekuwa akisafiri hapa na pale.
Alitawazwa/wekwa wakfu kuwa mtumishi wa Mungu mwaka 1939 akiwa na miaka 21 tu.
Alipata nafasi ya kuhubiri injili pande zote za dunia hadi Korea kaskazini na mkutano mkubwa aliowahi kuufanya ni ule wa Haringay Arena, London alioufanya mwaka 1954 ambao ulihudhuriwa na watu zaidi ya 12,000
Katika watu waliosikitishwa na msiba huu ni Raisi wa Taifa la Marekani, Bwana Donald TRUMP ambapo ameTWEET:
"Mtu mkubwa Billy Graham amefariki. Hakukuwa na mtu kama yeye! Atakumbukwa na wakristo na dini zote. Ni mtu wa kipekee"
Pumzika kwa amani mtu wa Mungu na God's General, BILLY GRAHAM.
0 comments: