UPDATES SAKATA LA KAKOBE: BAADA YA UCHUNGUZI, T.R.A YATOA RIPOTI


DAR: Mamlaka ya Mapato(TRA) imetoa Matokeo ya Uchunguzi kuhusu kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Church, Zachary Kakobe kusema ana pesa kuliko Serikali

TRA imesema Askofu Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha nchini. Katika akaunti ya Kanisa ambayo Kakobe ni mmoja wa Wasimamizi wamekuta shilingi 8,132,100,819.00

Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika kampuni za kukuza mitaji. Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi.

Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na 'majaba' kinyume na taratibu za utunzaji fedha. Pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika

Aidha, Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi wa fedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini

SOURCE: JAMIIFORUMS

0 comments:

Copyright © 2018 iCHURCH Magazine