STORI YA MAJOR 1: HARAKA ZA MIPANGO YETU Vs BARAKA ZA MUNGU ZA MUDA MREFU
Nabii Shepherd Bushiri (kushoto) akimsikiliza baba yake wa kiroho Nabii Uebert Angel katika moja ya ibada walizofanya. |
Kama kawaida iCHURCH BLOG huwa tunakuletea makala na post za watumishi wa Mungu kutoka katika mitandao ya kijamii ambazo zinakuwa na mengi ya kufundisha, kufurahisha, kutupa changamoto, kuburudisha na kuongeza imani zetu pia.
Leo tupo na Nabii Bushiri (MAJOR 1) ambapo tarehe 8/2/2018 aliamua kushare na sisi stori fupi ambayo ililenga kutufundisha juu ya HARAKA tunazokuwa nazo wanadamu kutaka kutatua matatizo yetu VS BARAKA za Mungu za Muda mrefu.
Nabii Bushiri amejaribu kuonyesha namna gani huwa tunapishana na baraka za muda mrefu alizotupangia Mungu kwa kufanya uchaguzi wa kuangalia hapa karibu na sio mbali maishani.
Katika post hiyo aliandika yafuatayo:
"Je, mnajua wapendwa kwamba wakati mwingine katika kutafuta suluhisho za haraka kwa hali zetu za sasa na zinazotusumbua, tunaishia kupoteza baraka za muda mrefu ambazo Mungu ametuhifadhia?
Mimi nitakuambia stori hii.
"Wakati nipo Malawi, huduma yangu ilikuwa, kama ilivyo leo, inakua kila siku. Ili kuwafikia hata wale walio mbali, nilianzisha Prophetic Channel. Sasa, kuendesha televisheni, hasa kwenye satellite na ubora wa picha bora, inahitaji pesa nyingi. Kwa bahati mbaya, sikuwa na za kutosha. Nilihitaji kuongezewa.
"Nilimpigia baba yangu wa kiroho, Nabii Eubert Angel, @uebertangel kwa msaada. Aliniagiza niende Zimbabwe, ambako alikuwa wakati huo. Nilihisi kupata afadhali kwa sababu nilijua kwamba atasaidia.
"Hata hivyo, hisia hizo za afadhali zilikuwa kwa muda mfupi. Nilipofika nyumbani kwake, alinipeleka haraka kwenda chumbani mwake. Kulikuwa na mambo mawili juu ya kitanda chake: Moja, Bunda la hela $100 000 (zaidi ya milioni 220,000 Tsh) na chupa ya mafuta ya upako.
"Baada ya kuona fedha, nilihisi matatizo yangu yametimizwa mpaka alipokonya koo na akauliza ni kipi kati ya wawili, nilipaswa kuchagua. Nilichanganyikiwa.
"Katika hali yangu ya kuchanganyikiwa, hata hivyo nilikuwa na tahadhari. Nilipaswa kufanya uchaguzi wenye busara kwa sababu uamuzi huo, dhidi ya tatizo la haraka na kubwa ambalo nilikuwa nalo, litakuwa na njia ndefu katika ukuaji wa huduma yangu. Wakati nipo pale niliona ufunuo: Niliweza kuona kwamba nyuma ya fedha, sikuweza kuona mafuta ya upako; lakini nyuma ya mafuta ya upako, niliweza kuona pesa.
"Nilichagua mafuta ya upako na nikarudi Malawi kwa kimya.
"Miaka baadaye, baba yangu wa kiroho, Nabii Angel, alinikumbusha kuhusu tukio hili kwa sababu ya jinsi Mungu amebariki huduma yangu. 'Kumbuka uchaguzi wa hekima uliyofanya siku hiyo', alisema.
"Kwahiyo wapendwa, kila wakati ninapowaelekeza kuchukua mafuta yako na kujianoint wewe mwenyewe, sifanyi hivyo kwa mazoea bali kwa imani. Nimeona ni kazi kwangu na inaweza pia kufanya kazi kwako!"
Umepata somo? USIACHE KUCOMMENT ulichopata katika stori yake hii.
Be blessed...
0 comments: