WAPINGA KRISTO WAZIDI KUSUMBUA VYUONI MAREKANI
NEW YORK
Kundi la watu
wasioamini Mungu wanaotambulika kama ATHEIST, wamekitaka chuo kimoja nchini
marekani kuondoa misalaba iliyopo katika majengo yake.
Ilielezwa kuwa chuo
cha New Mexico kilikuwa na misalaba kadhaa ikionesha uwepo wa Imani ya Kikristo
lakini kundi hilo lilishinikiza kuondoa likidai kuwa kwasababu chou hicho sio
cha kidini, sio sahihi kuweka alama za misalaba.
Wapinga Mungu
hao kupitia uongozi wake walituma barua kwa raisi wa chuo hicho bwana Kelvin
Sharp, wakitaka kusiwepo na alama zozote za kidini kwenye maeneo ya chou hicho
kwasababu yanamilikiwa na umma.
alama ya msalaba ukiwa mlangoni mwa ofisi za chuo hicho |
“Tunafahamu kuwa
chou cha New Mexico Junior kina misalaba kadhaa inayoonekana. Tunaelewa kuwa
kuna misalaba kwenye sehemu za mapokezi n ahata ofisi ya mhasibu.” Barua ilisomeka
hivyo.
Barua hiyo
ilieleza kuwa kuweka misalaba kwenye maeneo ya umma ni kinyume na katiba ya
nchi hiyo.
0 comments: