MAJOR 1 KUZINDUA MRADI HUU MKUBWA SIKU YA BIRTHDAY YAKE TAREHE 20 FEBRUARY
Karibu masaa manne yaliyopita, Nabii Shepherd Bushiri maarufu kama "MAJOR 1" ameweka wazi/bayana kuhusu ni lini atazindua moja kati ya miradi ambayo anajisikia fahari kuitimiza.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, nabii huyo na kiongozi wa kanisa la ECG, aliandika kuwa atazindua Hoteli yake mpya na ya kisasa tarehe 20 mwezi februari ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Haya ni maneno yake:
"Shepherd Bushiri Hotels, Sparkling waters and Spa, imepangwa kufunguliwa siku ya kuzaliwa yangu, Februari 20. Chini ni mtazamo wa mambo ya ndani ya mgahawa huu.
"Ilikuwa ni ndoto wakati nilipoanza mradi huu lakini sasa ni dhahiri. Hoteli hii inaongezea hoteli zetu zilizopo duniani kote, jumla ya 8. Kati ya nane, tatu zilizopo nchini Marekani zitazinduliwa siku chache kutoka sasa.
"Hebu niwahimize/niwatie moyo kuendelea kuamini katika ndoto zako, bila kujali ni kubwa kiasi gani. Hata kama watu wengine watacheka kwenye imani yako kufikiri kuwa haiwezekani, hawajui kwamba kwa Mungu wetu ni INAWEZEKANA.
"Karibu kwenye SB HOTELS, SPARKLING AND HOT SPA.
Pokea neema ya mali katika jina la Yesu!"
TUMEKUWEKEA PICHA ZA MRADI HUO:
0 comments: