USHIRIKINA: MDADA AUNGUZWA KWA MOTO NA WAGANGA ILI APATE UJAUZITO
RORYA, MARA: Jeshi la Polisi linawashikilia waganga wa jadi wawili kwa tuhuma za kumuunguza kwa moto Emiliana Thomas mwenye tatizo la kutopata ujauzito
Waganga hao walimwambia Emiliana kuwa ili apate mtoto ni mpaka kuku amwagiwe mafuta ya taa na ateketezwe kwa moto huku mama huyo akiwa amemshikilia mikononi
Kamanda wa Polisi, Henry Mwaibambe alisema waganga hao walimweleza mwanamke huyo kuwa anasumbuliwa na mashetani ndani ya tumbo na ndio yanayomfanya asizae, hivyo kuku akiteketea mikononi mwake atakuwa ameondokana na mashetani
Aidha, Mwaibambe amesema hali ya mama huyo ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kowak wilayani humo
TUMWAMINI MUNGU JAMANI. Neno lake linasema kuwa TUNAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA.
SOURCE: JAMIIFORUMS
0 comments: