Askofu wa
dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga na Simiyu), Dk.
Emmanuel Makala ataweka rekodi katika utumishi wake kutokana na mpango wake wa
kutembea kilometa 340 kwa lengo la kuujenga Ufalme wa Mungu.
Dk. Makala ataanza
matembezi hayo ya majuma mawili machi 18 katika usharika wa Neema Lamadi na
kumaliza Aprili 1 katika usharika wa Agape uliopo kahama.
Matembezi ya
Askofu huyo yanalenga kukusanya fedha, Zaidi ya shilingi milioni 120 za
maendeleo ya misioni za dayosisi hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali kutokana na kuwa ni eneo ambalo lina mauaji ya albino na vikongwe.
Mojawapo ya
mambo atakayofanya katika matembezi hayo ya miguu ni pamoja na kuendeleza kazi
ya injilli, kukemea mauaji ya albino na kusisitiza watu kufanya kazi kwa bidii.
KILA LA KHERI
ASKOFU.
SOURCE: UPENDO
MEDIA
Maelfu ya
wakristo nchini Marekani wamekusanya sahihi zao kupendekeza kuwepo kwa siku
maalum ya kitaifa kila mwaka kwa ajili ya hafla ya kumuenzi mwinjilisti Billy
Graham.
Graham,
aliyefariki mapema Februari 21, 2018 alikuwa akihubiri katika nchi mbalimbali
duniani, na kuwa mwalimu na mhamasishaji wa wanaofanya huduma hiyo katika
maeneo mengineyo ikiwemo barani Afrika.
Katika mazishi
yake, ilielezwa kuwa watu Zaidi ya 2000 walihudhuria wakiwemo viongozi wakuu wa
serikali na familia zao kama Raisi Donald Trump aliyekwenda na mkewe Melania
Trump.
Hatua hiyo ya
kukusanya sahihi kupendekeza kuwepo kwa kumbukumbu ya Graham ilikuja hivi
karibuni ikiongozwa na tovuti ya www.change.org
ambapo wakristo Zaidi ya 60,000 tayari wamekwisha saini kuunga mkono pendekezo
hilo.
Ilielezwa kuwa
baada ya kukusanywa kwa idadi kubwa ya sahihi hizo, zitawasilishwa kwa Raisi
Trump ili kusikiliza maamuzi yake juu ya pendekezo hilo. Endapo Trump ataruhusu
kumbukumbu ya mwinjilisti huyo, maana yake nchini Marekani kutakuwa na siku
maalumu kitaifa kama siku kuu nyingine kwa ajili ya kumuenzi mtumishi huyo wa
Mungu.
SOURCE: UPENDO
MEDIA
Nabii Shepherd Bushiri akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake katika hafla hiyo |
Muonekano wa ndani: sehemu ya ukumbi kwa ajili ya shughuli mbalimbali |
wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini kinachoendelea |
Muonekano wa nje. |
Mwakilishi wa kutoka ikulu akiwasilisha ujumbe kutoka ikulu |
Meneja mkuu wa hoteli hiyo akikaribisha wageni waalikwa |
What a Logo!!!! |
MAJOR 1 akitoa hotuba |
Muonekano wa nje wa hoteli hiyo |
Nabii Bushiri akifurahia jambo |
muonekano: sehemu ya nje kibarazani |
Hakika inapendeza |
Mkurugenzi wa Hoteli hiyo Bwana David Dix akitoa neno la ufunguzi wa tafrija hiyo |
Mafikizolo jukwaani wakiburudisha |
Mfalme wa RnB nchini Afrika ya Kusini, Bwana Donald, naye alioata wasaa wa kuimba |
Kundi la muziki la Mafikizolo wakitumbuiza katika tafrija hiyo |
Ni muda wa kuserebuka na kufurahia mafanikio |
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Brenden Praise alipata nafasi ya kumwimbia Mungu katika tafrija hiyo |
Nabii Bushiri akiwa na Baba yake wa kiroho, Nabii Uebert Angel |
|
|
wageni waalikwa katika hafla hiyo |
Muonekano wa ndani ya hoteli hiyo |
NORTH CAROLINA, MAREKANI:
Mhubiri wa Kimataifa, Mchungaji Billy Graham(99) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake
Mchungaji huyo amefikwa na mauti baada ya kuugua magonjwa kadhaa ikiwemo Saratani ya tezi dume na Kiharusi
Graham amewafikia watu wengi na injili kupitia Tv na alikuwa mtumishi wa kwanza kutumia njia hiyo. ..
Alizaliwa 1918 na kukulia kitongoji cha Charlote, North Carolina na aliamua kuwa mkristo anayemaanisha akiwa na miaka 16 baada ya kusikia injili kutoka kwa mwinjilisti aliyekuwa akisafiri hapa na pale.
Alitawazwa/wekwa wakfu kuwa mtumishi wa Mungu mwaka 1939 akiwa na miaka 21 tu.
Alipata nafasi ya kuhubiri injili pande zote za dunia hadi Korea kaskazini na mkutano mkubwa aliowahi kuufanya ni ule wa Haringay Arena, London alioufanya mwaka 1954 ambao ulihudhuriwa na watu zaidi ya 12,000
Katika watu waliosikitishwa na msiba huu ni Raisi wa Taifa la Marekani, Bwana Donald TRUMP ambapo ameTWEET:
"Mtu mkubwa Billy Graham amefariki. Hakukuwa na mtu kama yeye! Atakumbukwa na wakristo na dini zote. Ni mtu wa kipekee"
Pumzika kwa amani mtu wa Mungu na God's General, BILLY GRAHAM.
DAR: Mamlaka ya Mapato(TRA) imetoa Matokeo ya Uchunguzi kuhusu kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Church, Zachary Kakobe kusema ana pesa kuliko Serikali
TRA imesema Askofu Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha nchini. Katika akaunti ya Kanisa ambayo Kakobe ni mmoja wa Wasimamizi wamekuta shilingi 8,132,100,819.00
Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika kampuni za kukuza mitaji. Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi.
Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na 'majaba' kinyume na taratibu za utunzaji fedha. Pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika
Aidha, Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi wa fedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini
SOURCE: JAMIIFORUMS
RORYA, MARA: Jeshi la Polisi linawashikilia waganga wa jadi wawili kwa tuhuma za kumuunguza kwa moto Emiliana Thomas mwenye tatizo la kutopata ujauzito
Waganga hao walimwambia Emiliana kuwa ili apate mtoto ni mpaka kuku amwagiwe mafuta ya taa na ateketezwe kwa moto huku mama huyo akiwa amemshikilia mikononi
Kamanda wa Polisi, Henry Mwaibambe alisema waganga hao walimweleza mwanamke huyo kuwa anasumbuliwa na mashetani ndani ya tumbo na ndio yanayomfanya asizae, hivyo kuku akiteketea mikononi mwake atakuwa ameondokana na mashetani
Aidha, Mwaibambe amesema hali ya mama huyo ni mbaya na anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kowak wilayani humo
TUMWAMINI MUNGU JAMANI. Neno lake linasema kuwa TUNAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA.
SOURCE: JAMIIFORUMS
Karibu masaa manne yaliyopita, Nabii Shepherd Bushiri maarufu kama "MAJOR 1" ameweka wazi/bayana kuhusu ni lini atazindua moja kati ya miradi ambayo anajisikia fahari kuitimiza.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, nabii huyo na kiongozi wa kanisa la ECG, aliandika kuwa atazindua Hoteli yake mpya na ya kisasa tarehe 20 mwezi februari ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Haya ni maneno yake:
"Shepherd Bushiri Hotels, Sparkling waters and Spa, imepangwa kufunguliwa siku ya kuzaliwa yangu, Februari 20. Chini ni mtazamo wa mambo ya ndani ya mgahawa huu.
"Ilikuwa ni ndoto wakati nilipoanza mradi huu lakini sasa ni dhahiri. Hoteli hii inaongezea hoteli zetu zilizopo duniani kote, jumla ya 8. Kati ya nane, tatu zilizopo nchini Marekani zitazinduliwa siku chache kutoka sasa.
"Hebu niwahimize/niwatie moyo kuendelea kuamini katika ndoto zako, bila kujali ni kubwa kiasi gani. Hata kama watu wengine watacheka kwenye imani yako kufikiri kuwa haiwezekani, hawajui kwamba kwa Mungu wetu ni INAWEZEKANA.
"Karibu kwenye SB HOTELS, SPARKLING AND HOT SPA.
Pokea neema ya mali katika jina la Yesu!"
TUMEKUWEKEA PICHA ZA MRADI HUO:
Nabii Shepherd Bushiri (kushoto) akimsikiliza baba yake wa kiroho Nabii Uebert Angel katika moja ya ibada walizofanya. |
Kama kawaida iCHURCH BLOG huwa tunakuletea makala na post za watumishi wa Mungu kutoka katika mitandao ya kijamii ambazo zinakuwa na mengi ya kufundisha, kufurahisha, kutupa changamoto, kuburudisha na kuongeza imani zetu pia.
Leo tupo na Nabii Bushiri (MAJOR 1) ambapo tarehe 8/2/2018 aliamua kushare na sisi stori fupi ambayo ililenga kutufundisha juu ya HARAKA tunazokuwa nazo wanadamu kutaka kutatua matatizo yetu VS BARAKA za Mungu za Muda mrefu.
Nabii Bushiri amejaribu kuonyesha namna gani huwa tunapishana na baraka za muda mrefu alizotupangia Mungu kwa kufanya uchaguzi wa kuangalia hapa karibu na sio mbali maishani.
Katika post hiyo aliandika yafuatayo:
"Je, mnajua wapendwa kwamba wakati mwingine katika kutafuta suluhisho za haraka kwa hali zetu za sasa na zinazotusumbua, tunaishia kupoteza baraka za muda mrefu ambazo Mungu ametuhifadhia?
Mimi nitakuambia stori hii.
"Wakati nipo Malawi, huduma yangu ilikuwa, kama ilivyo leo, inakua kila siku. Ili kuwafikia hata wale walio mbali, nilianzisha Prophetic Channel. Sasa, kuendesha televisheni, hasa kwenye satellite na ubora wa picha bora, inahitaji pesa nyingi. Kwa bahati mbaya, sikuwa na za kutosha. Nilihitaji kuongezewa.
"Nilimpigia baba yangu wa kiroho, Nabii Eubert Angel, @uebertangel kwa msaada. Aliniagiza niende Zimbabwe, ambako alikuwa wakati huo. Nilihisi kupata afadhali kwa sababu nilijua kwamba atasaidia.
"Hata hivyo, hisia hizo za afadhali zilikuwa kwa muda mfupi. Nilipofika nyumbani kwake, alinipeleka haraka kwenda chumbani mwake. Kulikuwa na mambo mawili juu ya kitanda chake: Moja, Bunda la hela $100 000 (zaidi ya milioni 220,000 Tsh) na chupa ya mafuta ya upako.
"Baada ya kuona fedha, nilihisi matatizo yangu yametimizwa mpaka alipokonya koo na akauliza ni kipi kati ya wawili, nilipaswa kuchagua. Nilichanganyikiwa.
"Katika hali yangu ya kuchanganyikiwa, hata hivyo nilikuwa na tahadhari. Nilipaswa kufanya uchaguzi wenye busara kwa sababu uamuzi huo, dhidi ya tatizo la haraka na kubwa ambalo nilikuwa nalo, litakuwa na njia ndefu katika ukuaji wa huduma yangu. Wakati nipo pale niliona ufunuo: Niliweza kuona kwamba nyuma ya fedha, sikuweza kuona mafuta ya upako; lakini nyuma ya mafuta ya upako, niliweza kuona pesa.
"Nilichagua mafuta ya upako na nikarudi Malawi kwa kimya.
"Miaka baadaye, baba yangu wa kiroho, Nabii Angel, alinikumbusha kuhusu tukio hili kwa sababu ya jinsi Mungu amebariki huduma yangu. 'Kumbuka uchaguzi wa hekima uliyofanya siku hiyo', alisema.
"Kwahiyo wapendwa, kila wakati ninapowaelekeza kuchukua mafuta yako na kujianoint wewe mwenyewe, sifanyi hivyo kwa mazoea bali kwa imani. Nimeona ni kazi kwangu na inaweza pia kufanya kazi kwako!"
Umepata somo? USIACHE KUCOMMENT ulichopata katika stori yake hii.
Be blessed...
NEW YORK
Kundi la watu
wasioamini Mungu wanaotambulika kama ATHEIST, wamekitaka chuo kimoja nchini
marekani kuondoa misalaba iliyopo katika majengo yake.
Ilielezwa kuwa chuo
cha New Mexico kilikuwa na misalaba kadhaa ikionesha uwepo wa Imani ya Kikristo
lakini kundi hilo lilishinikiza kuondoa likidai kuwa kwasababu chou hicho sio
cha kidini, sio sahihi kuweka alama za misalaba.
Wapinga Mungu
hao kupitia uongozi wake walituma barua kwa raisi wa chuo hicho bwana Kelvin
Sharp, wakitaka kusiwepo na alama zozote za kidini kwenye maeneo ya chou hicho
kwasababu yanamilikiwa na umma.
alama ya msalaba ukiwa mlangoni mwa ofisi za chuo hicho |
“Tunafahamu kuwa
chou cha New Mexico Junior kina misalaba kadhaa inayoonekana. Tunaelewa kuwa
kuna misalaba kwenye sehemu za mapokezi n ahata ofisi ya mhasibu.” Barua ilisomeka
hivyo.
Barua hiyo
ilieleza kuwa kuweka misalaba kwenye maeneo ya umma ni kinyume na katiba ya
nchi hiyo.
NAIROBI
Shule ya
sekondari ya JAMUHURI nchini Kenya imetajwa kuwa na sintofahamu kwa wakristo
baada ya mwanafunzi mmoja kushambuliwa kwa kisu baada ya kukataa kubadili dini
kuwa Muislamu.
Ilielezwa kuwa
wakati wa usiku, mwanafunzi huyo wa kiislamu alikuwa akiuchambua uislamu na
baadaye kuanza kumshawishi aliye jirani naye akane ukristo awe Muislamu na
alipokataa ndipo alipomshambulia kwa kisu.
“Kuna mwenzetu
yeye ni muislamu alikuwa analazimisha na sisi tulio wakristo tukiri Imani yake,
na aliyekataa ndio humchoma kisu na wengine kuwapiga” mmoja wa mashahidi wa
tukio hilo alisema.
Taarifa
iliyotolewa na tovuti ya christianheadline, ilieleza kuwa shule hiyo iliyoko
kaskazini mwa mji wa Nairobi ina ushawishi mkubwa wa makundi ya Kiislamu kutoka
nchini Somalia hali inayotishia usalama wa wanafunzi walio waumini wa Kikristo.
Ilielezwa kuwa
miezi kadhaa iliyopita, kutokana na ubaguzi uliopitiliza unaofanywa na
wanafunzi wa kiislamu dhidi ya wakristo, Uongozi wa shule uliamua kutenga
mabafu na vyumba vya maktaba ili kuwaweka katika majengo tofauti kuepuka
madhara yanayoweza kuchochewa na ubaguzi huo.
Tovuti ya
Morning Star ilieleza kuwa wanafunzi wamekuwa wakinunua visu na mapanga kwa
ajili ya kutekeleza uhalifu ndani ya shule hiyo, wakiwalenga waamini wa Kristo.
Katika tukio
hilo wanafunzi wengine 15 walijeruhiwa na mamlaka zimeamuru shule hiyo kufungwa
wakati polisi wakiendelea na upelelezi kuwabaini wanaochochea vurugu hizo.
SOURCE: UPENDO MEDIA
Mtumishi C.S Upthegrove alipomtembelea Nabii T.B Joshua
nchini Nigeria.
|
Mtumishi wa MUNGU ambaye alipata kuwekwa kwenye list ya watumishi wa Mungu waliotikisa Ulimwengu kwa kuhubiri na kudhihirisha uwepo na nguvu za Mungu, C.S Upthegrove amefariki dunia.
C.S Upthegrove amefariki mnamo jumapili ya tarehe 28 januari 2018 akiwa nyumbani mwake huku akiwa kazungukwa na ndugu, jamaa, na marafiki.
Mtumishi huyo aliwahi kwenda nchini NIGERIA kumtembelea Nabii TB JOSHUA na kumweleza namna ambavyo amemuona na kuambiwa na Mungu kuja kumkabidhi vitu ambavyo viliachwa na God's General mwingine A.A ALLEN.
C.S Upthegrove amefariki akiwa na miaka 90. Alizaliwa 1928 na amefariki juzi 28/01/2018
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Emmanuel TV pamoja na Nabii TB JOSHUA wameandaa video hii fupi:
Jumapili ya tarehe 28/01/2018 ilikuwa ni jumapili ya tofauti sana na ya kukumbukwa kwa mchungaji Peter Mitimingi pamoja na waumini/wafuasi wake baada ya kufanya uzinduzi wa kanisa lao la WAREHOUSE CHRISTIAN CENTER (WHC) mitaa ya mwenge karibu na kituo cha mabasi cha "ITV".
Katika siku hiyo, matukio mengi yalifanyika na tunakuletea PICHA za matukio hayo kama ifuatavyo:
Timu ya kusifu na kuabudu ikihudumu |
Idara ya mapokezi walifanya kazi nzuri pia |
Wabeba maono wa kanisa la WCC katika picha ya pamoja |
Mch Mitimingi akizungumza na watoto waliohudhuria ibada hiyo |
Mch Mitimingi katika picha ya pamoja na vijana wa kanisa hilo hapo jana. |
Mch Mitimingi pamoja na mkewe Patience Mitimingi wakiwasalimia baadhi ya watu waliohudhuria ibada hiyo |
Jeshi la Polisi pia lilikuwepo kuhakikisha usalama unakuwepo hasa kutokana na wingi wa watu waliojitokeza |
Mch mitimingi akihubiri katika ibada hiyo |
Baba na mama mchungaji. walipendeza sana |
Muda wa kuabudu katika roho na kweli |
Kulikuwa na mabasi maalum ya kuwaleta watu na hapa yalikuwa yakiwashusha |
Wachungaji wakuu wakiingia ibadani |
Ni muda wa chakula cha Bwana. NENO LA MUNGU |
Mama mchungaji Patience Mitimingi akihudumu |
Mchungaji Mitimingi madhabahuni |
Media team |
Selfie zilipigika pia |
waliojitokeza walikuwa ni wengi mno |
Waumini waliohudhuria ibada hiyo wakifuatilia kwa ukaribu kinachoendelea ibadani |
Mchungaji Mitimingi akiingia eneo la tukio huku akisalimiana na vijana wahudumu wa siku hiyo maalumu |
Subscribe to:
Posts (Atom)